Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Mwezi huu Naibu Waziri Mkuu amepata msiba kwake, amefiwa na shemeji yake kijijini kwake Bulangwa, Jimbo la Bukombe ndio msiba umetokea wa Naibu Waziri Mkuu.
Kama kawaida, bwana kiongozi akija tunasimamishwa njiani masaa kadha wakadha huku tukisubiri apite huku uzalishaji ukiwa umesimama kumsubiri apite ndio turuhusiwe kuendelea na shughuli zetu.
Kiukweli kabisa toka ndani ya moyo wangu hili suala linanikera sana ni vile sina namna sababu tunaongozwa na watawala, na siyo viongozi.
Nikurudishe kwenye stori yetu kama kichwa kilivyojieleza hapo juu.
Bwana nyumbani kwake huyu Waziri akija tu, wanakijiji na majirani zake husogea kwake kumuomba msaada hii ni tabia imejengeka kila akija lazima watu wajae kwake kumomba msaada wa kifedha, wenye kuomba ada n.k mpaka atakapoondoka ndio na wao huondoka pale nyumbani kwake.
Na ni foleni kumuona pindi unapoenda, polisi hufanya kazi ya kupanga watu namna ya kumuona na husaidiana na wasaidizi wake.
Sasa basi kitu nachoshangaa hawa wananchi ni hii tabia ya kuwa ombaomba. Wanaume kwa wanawake hupiga kambi nyumbani kwa naibu Waziri Mkuu mpaka atakapoondoka na huwapikia wanakula na kusaza ndio maana wamezoea hivyo.
Najiuliza hili taifa tuna watu au kizazi cha aina gani hiki? Tumeshindwa kutumia nguvu na akili hata hizi za mkoloni kujikomboa tumekuwa kama mandondocha yaani mamisukule kwa kuwatumikia watu wenye navyo!!
Nina imani kabisa hili taifa tuliwahi tu kupata uhuru haikuwa sawa kupata miaka hiyo ilitakiwa sasa ndio tuombe au tungechelewa kidogo kuupata uhuru hiki ninachokishuhudia Mungu akiniweka salama sijui nitakijibu nini kizazi cha watoto wangu au kizazi cha vitukuu vyangu.
Maana wataona kama tulikuwa tunaujinga mwingi sana katika kizazi chetu cha karne yetu.
Sihitaji kunukuliwa vibaya kwamba nawatukana au laah lakini hiki nachokiona kinadumaza sana utafutaji kwa jamii hii inayomzunguka Naibu Waziri Mkuu.
Hii imeonyesha ni namna gani CCM inamtaji wa watu wasio na vision wala mawazo mbadala wanavyowatukuza viongozi wanaowachagua baadae hugeuka na kuwatukuza kama bila wao hawaishi au hawawezi fanya chochote.
Ikabidi niulize hii anayofanya anawezaje kuwaletea maendele kama Mh. Anawapikia na kuwa chinjia ng'ombe huoni anawapumbaza kwa chakula washindwe kuhoji maendeleo ya jimboni kwao?
Niko hapa Bukombe sioni maendeleo katika Wilaya hii iwe hapa hapa Ushirombo au Vijijini hakuna kinachofanyika cha maendeleo,
Mama mmoja nikamuuliza, Waziri toka ameingia kuliongoza jimbo hili nini amefanya cha maana au alikuta hakipo akafanya maana naona hakuna kitu cha maana kinachofanyika hapa?
Yule mama kindaki ndaki na shabiki au mfuasi wa CCM akasema yeye amejenga shule za msingi na sekondari akatoa mfano wa shule aliyoijenga Doto Biteko ni shule ya sekondari amejenga inaitwa DOTO BITEKO SEKONDARI SCHOOL nikasema basi inatosha nashukuru tukaachia hapo maongezi.
Miaka 60 ya uhuru unasema Doto kajenga shule ya sekondari tena kaandika jina lake na bado unasema umeletewa maendeleo?? CCM bado wapo sana kwenye hii nchi hawana mpinzani kabisa Mungu aendelee kutusaidia tu ambao tunahitaji uwajibikaji na hatuoni wawajibikaji.