Nataka nizae mapacha

Kama kwenu hakuna historia hiyo kweli ni ngumu, labda kama unataka mapacha wa kupandikizwa(kitaalam). Lakini kama inawezekana ungefikiria pia kuzaa at short intervals hao wawili zaidi unaowataka kisha ukatulia zako. Angalizo: Kuzaa at short intervals inabidi kuobserve the following: Good health,income,etc.
 
Anitafute mimi nitampa hizo dabodabo anazotaka, lakini washauriane na mumewe kwanza. Isijekuwa tabu baadae!
 
Mimi nami nilipenda sana Mke wangu tupate mapacha. Mzao wa kwanza tukapata mapacha 4 (sijui wanaitwaje, manake mapacha ni wawili, wakiwa wanne sijui), wakiume 3 na binti 1. Ila ilitokea tu hakukutumika dawa yoyote. Wakati wakiwa wachanga ilikuwa kazi kuwalea, ilibidi kweli nisitishe shughuli zangu zote nilizokuwa nafanya kumsaidia mamaa kulea. Lakini sasa wamekua kiasi raha sana ukiwaona.
 
Jamani nashururuni sana kwa ushauri na mawazo yenu mazuri. Ushauri wenu ni mzuri sana!!!
 
Jamani nashururuni sana kwa ushauri na mawazo yenu mazuri. Ushauri wenu ni mzuri sana!!!

umeridhika dada yangu lakini? kama bado husisite kurudi jamvini! kila la kheri
 
Jibu la WOS post namba 18 ndio sahihi. fuata hilo utapata tu.
Kwa wengine tumewapata kwa bahati tu wala hapta bila plan yoyote ile.
 
go for fertility treatment hapo utapata hata nane!!!!! Ocotomom mara moja!
 


Ovarian stimulations hormones wanazopewa akina mama wenye matatizo ya uzazi usababishwao na kukosekana kwa mayai husababisha mama kutoa mayai zaidi ya moja na hapa ndio mapacha wanapatikana. Dawa maarufu wanayoprescribe madaktari Tanzania ni Clomid, ziko na nyingine more aggresive kama Repronex, Menopur, Gonal-F, Follistim na Bravelle. Sijui kama madaktari watakubali kukupa hizi dawa wakati wewe huna matatizo ya uzazi. Zina mambo mengi mfano huwezi kutumia dawa ya aina moja zaidi ya cycle 3 na unahitaji ufuatiliaji wa vipimo kama ultrasound unless unapewa dozi ndogo mfano 50mg.

Hata hao wanaopandishwa kwa kutumia process za IVF wanatumia hormones kwanza kukuza mayai maana hii process inafanywa na mayai at least matatu kuincrease chances of success hasa ukitilia maanani process yenyewe ni ghali cycle moja $10,000 hadi $35,000 cycle 3.
 
N bora utosheke na uliye naye, shukuru Mungu then tulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…