Natakiwa kulipa kodi ya mapato TRA - biashara ndogo ndogo

Michosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
662
Reaction score
649
Mwaka jana mwezi wa 10,nilianzisha biashara yangu ndogo kulingana na mtaji mdogo nilokuwa nao.kabla ya kuanza nilienda TRA ili nipate TIN,kisha leseni ya biashara.Biashara hiyo ni STATIONERY.Utaratibu nilopitia kupata TIN ilibidi wanifanyie kwanza tathimini ya biashara yangu,na yule kija akanishauri kuwa ili nipate hiyo TIN inabidi tathinmini ya kipato changu kiwe kinanzia 18,000/= kwa siku.
lakini baada ya kuanza biashara kwa siku ilikuwa ni ngumu kufikisha hiyo Elfu 18,ikabidi nibadili eneo la biashara nako hali haiijakaa sawa,tatizo ni mtaji mdogo kwani sina daftari, kalamu wala bidhaa nyingine,ila nina type,print,photocopy,scanning na pia natoa huduma ya Mpesa na Tigo pesa basi,sina kitu kingine kabisa.
kodi ya mapato inatikiwa kulipwa,japo jamaa hawajanitembelea, lakini hiyo amount inayostaili mtu ufikie kiwango cha kulipa kodi sipati kwa siku.JE NIFANYE NINI,KABLA YA KURUDI KULE TRA NAOMBENI USHAURI WENU WADAU ILI NIPATE KUFAHAMU MENGI ZAIDI JUU YA KODI YA MAPATO KWA HAPA NCHINI HASA KWA BIASHARA NDOGO NDOGO.
 
pole mkuu yamenikuta kama yako ngoja watak uja wanaoelewa hii issue
 
Tupo wengi

MKUU,kwani hata wewe ni hivyohivyo?utaratibu mbona mie siuelewi,ndo maana nimekuja hapa kabla ya kurudi TRA,kwenye kitengo cha elimu kwa mlipa kodi ili kama kuna mtu anaye jua zaidi anieleweshe.
 
pole mkuu yamenikuta kama yako ngoja watak uja wanaoelewa hii issue

Dah,nikweli kaka km kuna mtu wa TRA hapa atupe elimu walau kidogo tu,tuondoe jam huko kwenye maofisi yao.
 
Kodi ya mapato kwa biashara ndogondogo inategemea makadirio uliyofanyiwa au unayofanyiwa na mtu wa TRA. Kwa mwaka wa fedha tulionao haya ndo mahesabu wayotumia kujua ni kiasi gani ulipe
TAX RATES FOR SMALL BUSINESSES
Income tax rates for small and medium enterprises are as follows:
Turnover (Shs) Tax Payable Per Annum (Shs)

0 – 4,000,000 NIL 35,000 or 1.1% of the turnover
4,000,001 – 7,500,000 100,000 or 2% of turnover in excess of 4,000,000
7,500,001 – 11,500,000 212,000 or 70,000 plus 2.5% of turnover in excess of 7,500,000
11,500,001 – 16,000,000 364,000 or 170,000 plus 3% of turnover in excess of 11,500,000
16,000,001 - 20,000,000 575,000 or 305,000 plus 3.5% of turnover in excess of 16,000,000

Kwa hiyo kama wakikudaria kuwa kwa mwaka biashara yako itaingiza shs. mil 10.5 kama mauzo, itabidi ulipe shs. 212,000/= kwa mwaka kama kodi ya mapato ya stationery yako kwa mwaka mzima.

Hivi ndivyo ninavyofanyiwa kila mwaka.
 
Km kwa mwaka ni 212,000 je unalipa yote kwa wakati mmoja hau nusu,nusu kila baada ya miezi mitatu
 
KRISITINA mimi huwa nalipa yote kwa mara moja, nafikiri ukitaka kulipa kwa awamu inawezekana ila sijawahi kuwaulizia wafanyakazi wa TRA juu ya uwezekano huo.
 
Poa mana nimefanya research,kodi ya mapato ulipwa mara nne kwa mwaka 30.12,30.03,30.6.30.09. Nlikuwa sijui km unaweza kulipa yote.
 
Mkuu @michosho

Kwa mujibu wa BAJETI YA SERIKALI 2012/2013 wafanyabiashara wadogo ambao mapatao yao ktk mauzo hayazidi milioni 3 kwa mwaka, wamesamehewa kodi, hivyo wawapaswi kulipa kodi hata sent 5.

Kwa maana nyingine wewe ni mmoja wa wafanyabiashara wadogo, hupaswi kulipa kodi ya mapato kwa mujibu wa Bajeti ya 2012/2013, kama ilivyoainishwa HAPA.


[TD="width: 594, colspan: 5"] Viwango vinavyopendekezwa [/TD]

[TD="width: 53"]
[/TD]
[TD="width: 199"] Thamani ya Mauzo [/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Kodi kwa wasiokuwa na kumbukumbu za mauzo
[/TD]
[TD="width: 159"]
Kodi kwa wenye kumbukumbu za mauzo
[/TD]

[TD="width: 53"] (i)
[/TD]
[TD="width: 199"] Kwa mauzo yasiyozidi Shs. 3,000,000/= [/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Asilimia sifuri (0%)
[/TD]
[TD="width: 159"] Asilimia sifuri (0%)
[/TD]

[TD="width: 53"](ii)[/TD]
[TD="width: 199"]Kwa mauzo yanayozidi Shs 3,000,000/= na yasiyozidi Shs 7,500,000/=[/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Shs. 100,000/=​
[/TD]
[TD="width: 159"]2% ya mauzo yanayozidi
Shs 3,000,000/=
[/TD]

[TD="width: 53"](iii)[/TD]
[TD="width: 199"]Kwa mauzo yanayozidi Shs 7,500,000/= na yasiyozidi Shs 11,500,000/=[/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Shs. 212,000/=​
[/TD]
[TD="width: 159"]Shs. 90,000/= plus 2.5% ya mauzo yanayozidi Shs 7,500,000/=
[/TD]

[TD="width: 53"](iv)[/TD]
[TD="width: 199"]Kwa mauzo yanayozidi Shs 11,500,000/= na yasiyozidi Shs 16,000,000/=[/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Shs. 364,000/=​
[/TD]
[TD="width: 159"]Shs. 190,000/= + 3.0% ya mauzo yanayozidi Shs 11,500,000/=[/TD]

[TD="width: 53"](v)[/TD]
[TD="width: 199"]Kwa mauzo yanayozidi Shs 16,000,000/= na yasiyozidi Shs 20,000,000/=[/TD]
[TD="width: 183, colspan: 2"]
Shs. 575,000/=​
[/TD]
[TD="width: 159"]Shs. 325,000/= + 3.5% ya mauzo yanayozidi Shs 16,000,000/=[/TD]


Sasa namna gani TRA wanaweza kupata makisio ya mauzo yako kwa mwaka, ni kupitia daftari lako la mauzo ya kila siku na kitabu chako cha risiti, ndipo wanajua kwa mwaka unaingiza sh ngapi.

Ila kwa wewe ambaye biashara yako bado changa kwa maana kwamba hujatimiza mwaka 1 ktk biashara ni wazi TRA hawawezi kukupigia hesabu kujua unapaswa kulipia kiasi gani, hivyo wanatakiwa wakuache kwa mwaka 1 bila kulipa kodi.

mfano kwa siku unaingiza shs 18,000/= ukitoa pesa ya chakula kwa siku sh 6,000/= unabakiwa na shs 12,000/=
shs 12,000*30 = shs 360,000/= = mapato kwa mwezi ila kodi ya chumba cha biashara kwa mwezi ni shs 150,000/= hivyo unabakiwa na shs 210,000/=
shs 210,000*12 = 2,520,000/=

Kwa maana hiyo mapato yako kwa mwaka yangekuwa sh 2,520,000/= hivyo hayazidi milioni 3, bado una haki ya kutokulipa kodi kwa mujibu wa BAJETI YA SERIKALI 2012/2013.
 

Mkuu umepambanua vizuri sana ila nataka kuongezea tu kwamba hili ulilolisema kwa kiasi kikumbwa haliangaliwi na TRA. Kwa vile wafanyabiashara wengi hawaweki kumbukumbu SAHIHI za biashara yao (hasa hawa wadogo wadogo), TRA wanakadiria kodi kulingana na mtaa unaofanyia biashara. Ipo mitaa ambayo wao wanaiona ina biashara, hivyo wanalazimisha ulipe kiwango fulani cha kodi.
 

Umeeza vizuri ila umepotosha mwishoni,
Niliuliza pale TRA kuhusu hili suala la wafanyabiashara wadogo,
Wamesema makadirio ya kodi hutegemea MAUZO kwa mwaka na sio faida.
Kwa mfano uliotoa ni kwamba 18,000 * 320days unapata 5,760,000 bila kutoa gharama yoyote ile.. Kwa hiyo kodi ni 100,000 kwa mwaka kwa kiwango hicho.
Soma vizuri.
Wanafanya hivi kwa kuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wadogo kuwa na records zinazotakiwa kama makampuni..
Ila kwa mwenye uwezo huo, makadirio hufanyika kutokana na jedwali lako kulia yaani kwa wenye kuweka kumbukumbu.
 


mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri. nashukru sana,kwani nimekuelewa.sasa,hawa jamaa wa TRA,niwasubili waje au niwafuate hukohuko kujihami mapema kabla hawajanikuta hapa kwenyye shughuli zangu????kwani ukweli ni kwamba hicho kiasi cha 4mil,kwa mwaka mie sifikishi na mbaya zaidi sina kumbukumbu nzuri za biashara yangu ambazo zinaweza kutumika kam reference,ndo nimeaaza kuweka kumbukukumbu ya vi-photocopy 10-15 ninavyopata kwa siku. hata kwa macho tu ukifika ofsini kwangu utabaini kuwa kwa siku siwezi kufikisha hicho kiasi(18,000/=),MWAZO MGUMU.
KITENGO HICHO CHA TRA,KWA MTAZAMO WANGU IDARA YA ELIMU KWA MLIPA KODI BADO HAIJASIMAMA VIZURI,,WAFANYABIASHARA WENGI HATUELEWI NA PENGINE WAJIPANGE ZAIDI KUTOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA WAPYA,NA WALIOPO ILI KUYPUNGUZ USUMBU WA KUHANGAISHANA NA WALIPA KODI.

 
Tatizo TRA wapo kwa ajili ya kumtisha na kumkomoa mfanyabiashara na siyo kumuelekeza na kumuelimisha ili apate kujua umuhimu wa kulipa kodi bika shuruti. TRA inatakiwa kumchukulia mlipa kodi kama mteja muhimu kwao hivyo basi kumuandalia mazingira mazuri ya kulipa kodi kwa moyo, lakini wao humjia mlipakodi kama ni mwizi na mhalifu, vitisho vingiiiiii kuliko kuelimisha, pyuuuu Tanzania
 
Kweli kabisa. Mmetuelezea vizuri. Na kwa kipindi iki anayestahili kuwa na EFD MACHINE ni mfanyabiashara wa aina gani? Mwenye kuingiza kiasi gani kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…