chatts55
JF-Expert Member
- Oct 11, 2012
- 600
- 97
Natumaini wote mpo salama,
Ni nani wa kumfunga paka kengere?
Na akitokea jasiri mmoja kati yetu kutaka kumfunga huyo paka kengere,je! ni mbinu gani atatumia?
Utendaji wa Wizara ya Elimu umekuwa hauridhishi kwa kipindi kirefu sasa,na wadau mbalimbali katika sekta ya Elimu wamepaza sauti kiasi cha kuomba maji kulainisha makoo yao.
Sipendezwi hata kidogo kwa namna wizara hii inavyoendeshwa,Sijui ni mfumo na vigezo gani vinavyotumika kurecruit wasomi kufanya kazi Wizarani.
Sasa hivi tunashuhudia kuibuka kwa Maafisa Elimu mbalimbali ambao naweza kusema ni "UCHWARA" kwa sababu hawajui misingi ya kazi zao.wanateuana aidha kwa kujuana au kwa kulipana fadhira.
Wakuu wa shule ndio usiseme,wanafanya mpaka kuhonga kupata ukuu huo.
Natamani sana nije niingie kufanya kazi wizara ya Elimu nikihodhi madaraka ya juu ili nifumue utumbo wote unaotendeka hivi sasa na kujenga uthabiti na ufanisi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi.
Mabadiliko yataletwa na mimi na wewe.
Tuunganishe nguvu zetu kutokomeza uozo katika elimu.