Natamani kufanya kazi wizara ya elimu

chatts55

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
600
Reaction score
97
Natumaini wote mpo salama,
Ni nani wa kumfunga paka kengere?
Na akitokea jasiri mmoja kati yetu kutaka kumfunga huyo paka kengere,je! ni mbinu gani atatumia?
Utendaji wa Wizara ya Elimu umekuwa hauridhishi kwa kipindi kirefu sasa,na wadau mbalimbali katika sekta ya Elimu wamepaza sauti kiasi cha kuomba maji kulainisha makoo yao.
Sipendezwi hata kidogo kwa namna wizara hii inavyoendeshwa,Sijui ni mfumo na vigezo gani vinavyotumika kurecruit wasomi kufanya kazi Wizarani.
Sasa hivi tunashuhudia kuibuka kwa Maafisa Elimu mbalimbali ambao naweza kusema ni "UCHWARA" kwa sababu hawajui misingi ya kazi zao.wanateuana aidha kwa kujuana au kwa kulipana fadhira.
Wakuu wa shule ndio usiseme,wanafanya mpaka kuhonga kupata ukuu huo.
Natamani sana nije niingie kufanya kazi wizara ya Elimu nikihodhi madaraka ya juu ili nifumue utumbo wote unaotendeka hivi sasa na kujenga uthabiti na ufanisi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi.
Mabadiliko yataletwa na mimi na wewe.
Tuunganishe nguvu zetu kutokomeza uozo katika elimu.
 

Omba Mungu utapata tu.
 
kwa jinsi ulivyoelezea tatizo la wizara hii kwa mtizamo wangu naona hata wewe ni wale wale hauna cha kufanya kusaidia. lazima ujue mfumo ukoje na tatizo liko wapi ndio unaweza kujaribu. lazima ujiulize anayeajiri watu ni nani? anayewasimamia watu wafanye kazi ni nani? anayepanga bajeti ya shughuli za kufanya ni nani? je tulikotoka kwa maana mfumo uliokuwepo unatatua matatizo yaliyopo na je tunataka kwenda wapi kwa mfumo gani au msukumo gani ukisha maliza haya yote ujiulize je coordinator wa haya maswala yote katika wizara ni nani? na je anafanya kazi yake ipasavyo? je anamamlaka ya kupanga, kuelekeza, kusimamia, kutunuku na kuwajibisha ?
 

Jibu ni hapana,unaweza mmbebesha zigo mtu mmoja wakati kuna delegation of power
 
Wanaotukana ovyo majukwaani n kuxma wenzao mafisadi wakat wenyewe wanamiliki meli ila mtazamo xory
 

That's it
 
Mwaarobaini wa wizara ya Elimu ni kuwa na sera mpya ya Elimu itakayotoa mwongozo wa mafunzo ulio na mfumo wa academic na profession oriented.Baada ya hapo ifanyike operesheni fumua kwa vigogo wote pale wizarani na kuweka damu mpya yenye maono hai,kwani wazee waliopo pale wizarani wapo kwamaslahi yao binafsi na kuhakikisha ndugu na jamaa zao wanakuwa na nafasi nzuri bilakujali uwezo wao wa kutekeleza mjukumu ya kazi.kuna watu wanaitwa maafisa Elimu wa wilaya na mikoa hawakuwahi kutumika darasani hawaijui kazi ya ualimu lakini leo ndio viongozi wa walimu mikoani na wilayani je kutakuwa na tija mashuleni? Au ndo sanaa na elimu kuendelea kuporomoka.Kwa kulihakiki hili wanajamii forum chunguzeni mawilayani mliko mtaona hao wnaoitwa maafisa elimu na utendaji kazi wao.
 

Tena ukizungumzia kuhusu maafisa elimu hadi inatia simanzi wengi ni mambulula wasio jua kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…