Natamani kujua sana hii kitu

Leomimi

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
2,547
Reaction score
872
Habari wapendwa, imekuwa ni kawaida na ndio naona ni kama style ya sasa kina dada kutongoza wanaume najiuliza hivi ni wadada wangapi waliotongoza wanaume na wakafanikiwa kimapenzi.

Na wakaolewa na hao wanaume mpaka leo mapenzi yao yapo strong hata kama JF wapo embu njooni mtupe uzoefu wenzenu ambao hatujawahi kufanya hivyo labda ni kwa ushamba au sio utamaduni karibuni MMU .
 
Kutongozwa siyo dhambi bwana ni raha pia au mpaka upige swaga uzungushwe ndo uamini unapendwa hapana mkuu ukitongozwa tena furahi afu kubali usikatae utapenswa we mpaka bas
 
Wanaume wengi wanachukulia ukicheche mdada akimtongoza wanapenda wao watongoze
 
Mie mwanafunzi alinambia, waweza nisubiri nimalize chuo unioe? Sikumjibu kitu, sasa ni miaka kumi na tano kama mke ni mme.
 
Kuna mwanaume nilimtokea humu humu Jf... Kwa raha zetu saivi ni mke na mume...!

Usione noma wee muimbishe tuu huyo jamaa mpaka akuelewe..!!
 

Mwambie ukweli kuwa unampenda au unatamani kuwa na awe baba wa watoto wako, ukishndwa onesha vitendo mfano. Mtumie picha mbali mbali za watoto au familia huku ukisindikiza picha hzo na ujumbe mzuri utashawish kuelewa lengo lako, ukishindwa pia anzisha urafiki tu wa kawaida then mdadisi fantasy yake kisha anzia hapo, ukishindwa pia tafuta ndugu au rafki anaelewana nae ujenge mazoe na huyo rafiki kisha utamtumia kufanikisha malengo yako

Cha muhimu ni kujiamini na usikilize moyo wako.

Fanya yafuatayo baada ya kufanikiwa kumpata
1. Unesha mapenzi kwa vitendo
2. Usiige maisha, ishi maisha yako ya kawaida tu
3. Usitamani visivyowezekana
4. Mpe ushauri wa maendeleo hasa mshaur juu ya kuwekeza na kujiendeleza kibiashara, kitaaluma na vingine vingi tu
5. Mtembelee kwake fanya shughuli ambazo hakutegemea kama utafanya

Hayo ni mawazo yangu

*** USITHUBUTU KUTUMIA WAGANGA KAMA UNA HAJA NA MAHUSIANO YA DHATI NA YA KWELI YENYE HAMANI NA FURAHA.
MTANGULIZE MUNGU KWA KILA JAMBO.

UKIFANIKIWA KUMPATA "USIBADILIKE"
kila lakheri
 
Jamani hebu mwageni mauhondo vizuri....kwa hiyo mwanaume wakati wa mtongozo huwa anasugua vidole au? manake unaweza kuuvamia uso wa mbuzi unakukata jicho mpaka unasahau maneno....lol.
Halafu kuhusu majibu vipi? Na wao wana zile swaga za "nipe muda nikafikirie" au wanakubali hapo hapo?
Halafu mechi ya ufunguzi nani huwa anatoa mwaliko?
Hebu mwageni madata jamaniii.....!
 
Mimi yashanikuta sana haya ya kutongozwa!kuna wadada ni makauzu acha tu!wanaimbisha kushinda wanaume, halafu sasa inafika point hadi unamkwepa yaani inakuwa kama kero!...
 
Jaman hodi hodi nasikia mnajadili kitu...loading error...
 

hahahahaaaaa process ni zile zile inabidi ww ndo utoe mwaliko kwny ufunguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…