Natamani kumuona Greenwood katika taswira ya Halaand

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Kalamu yangu imetapakaa vumbi, imepita miezi sikuweza kuitumia.

Kuna mengi yametokea katikati, yapo yaliyofurahisha na kuhuzunisha.

Yapo yaliyokonga nyoyo na kubugudhi, mwili wangu ulikufa ganzi.

Ni kama Samaki yasafirishwayo machozi yake na mawimbi ya bahari, ana mengi ya kusema lakini shehena ya maji kinywani mwake.

Leo nimeikumbuka Kalamu yangu, pengine huyu ndie mpenzi wangu wa kweli kuliko wapenzi wengine.
Mapenzi yangu kwake hayafichiki, ukweli wake kwangu haupingiki.

Ni yeye pekee ambae azijuae hisia zangu, ni yeye pekee ambae hakuwahi kunichoka.
Ni yeye pekee ambae siku zinakwenda bila kufanyika miamala kati yetu.

Mnalisikia jina la Haaland huko kwenu?, huku kwetu limetapakaa kila mahali.

Kwenya magazeti, kwenye mitandao ya kijamii, kulia na kushoto anazunguzwa kijana huyu mzaliwa wa Norway.

Uhodari wake wa kupachika mabao unampa umaarufu kila uchao, si mzuri wa kusukumana ila ni bora katika kuusukuma mpira nyavuni.

Ukiacha kumeza mate kufunga mabao ni kazi nyengine nyepesi mbele ya Haaland.

Huko kwenu mnamfahamu Mason Greenwood?, huku kwetu tunamjua kinaga ubaga.

Moja ya vijana ambao tunamtabilia makubwa juu yake.

Uhodari wake wa kufunga mabao ni kitu kengine kinachompa sifa kijana huyu.

Natamani kuiona taswira ya Haaland mbele ya Greenwood, kwanini?.

Haaland yupo Dortmund, ni sehemu salama kwake na kwa mustakabali wa kipaji chake.
Anacheza kwa nafasi, hana presha si ndani wala nje ya uwanja.

Greenwood yupo United, si sehemu salama kwake na kwa mustakabali mzuri wa kipaji chake.

Ni ngumu kwa Greenwood kuaminiwa na United, kwa sasa wanawaza akina Ighalo na wengineo.

Sioni nafasi ya Greenwood kikosini, itakuwa ni ngumu kwake kucheza kila siku katika timu yenye presha ya mashabiki.

Nilielewa kwanini wasimamizi wa Haaland walizikataa ofa za timu kubwa, walihitaji kumuona kijana huyo akikuwa zaidi.

Walihitaji kumuona Haaland anacheza dakika nyingi kama tumuonavyo sasa.

Vipi kwa Greenwood?, je anapata dakika nyingi kama afanyiwavyo Haaland?, jibu baki nalo.

Najua United wana mipango ya muda mrefu na Greenwood.

Natamani kuona wakimpeleka kwa mkopo katika timu ambayo atacheza kwa nafasi.

Katika timu ambayo haina presha ya mashabiki na msukumo wa kupata matokeo mazuri kila washukapo dimbani.

Hii itamjenga na kumkomaza zaidi Greenwood kitu ambacho Haaland anakipata hivi sasa.

Yangu ni hayo, sasa nairudisha Kalamu yangu kabatini.

EID MUBARAQ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andiko zuri. Unavyoona timu gani inamfaa mkopo?

Sent using motorola
 
Uandishi murua kabisa wa makala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado umri ni mdogo na kama nafasi amepewa sana this season..Hakuna timu kubwa ambayo ingempa nafasi kubwa hivi..Sio kila kinda anaweza kuingia first eleven fasta hivyo
 
YOUTH, COURAGE, SUCCESS.​

Kwa kampeni hii ya sasa Manchester United ikiongozwa na Solskjaer, Greenwood ndio mmoja wa walengwa. Greenwood sio mchezaji tegemezi kwamba tunategemea kila mechi afunge.

Greenwood hata akienda hizo timu ambazo hazina pressure ndani na nje ya uwanja kwa umri wake ni ngumu kupata nafasi kama aliyopewa United msimu huu.

Ukiachana na pressure za mechi kwa timu nzima wakitegemewa walete matokeo chanya na wakishindwa basi lawama huwa za wote ila leo hii kuna wachezaji kama Fernandez hawakutani na maneno makali ya mashabiki kitu tunachotegemea ndio ana-deliver, kazi anayopewa anaitimiza na timu inapata mchango wake kisawasawa ila sasa mtu kama Pereira kweli unategemea asiwe na pressure yeye kama yeye kwa ule uchezaji wake?

Pressure kwa timu na mchezaji inakuja kutokana na mategemeo makubwa ya mashabiki juu ya mchezaji halafu anakuja kuharibu, sasa leo hii Greenwood anapendwa, hategemewi kutupeleka fainali ya Europa League, hategemewi kutupeleka top 4 hiyo pressure kubwa ya mashabiki anaipata wapi?

Ndani ya uwanja Greenwood ame-offer kuliko mategemeo ya mashabiki wengi, pressure ya mashabiki anakutana nayo vipi? Tumlaumu kwa lipi, ni kweli mashabiki wa United wana kelele kwa kuwa na mategemeo makubwa halafu mwisho wa siku wachezaji wanawaangusha lazima tuongee, sasa Greenwood hata hatukutegemea yeye ku-score goli 10+ msimu huu ila ka-score kwanini tumsumbue mtoto mdogo kama yule. Acha tupugizane kelele na hawa wakina Lingard.

GREENWOOD IS HERE TO STAY!!!
 
Kumfananisha Haaland na Greenwood ni kumkosea adabu Haaland.
 
Back
Top Bottom