Natamani kuona mechi ya Soka Wabunge Vijana wa UKAWA vs CCM Kabla ya Uchaguzi

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
2,837
Reaction score
1,679
Natamani kuelekea Uchaguzi Wabunge Wa Ukawa Vijana Kwa kushirikiana na Wabunge Vijana Wa CCM Vijana kucheza Mechi Mpira wa Miguu. Mechi hii ni ya kutuandaa Vijana Wa Tanzania Kisaikolojia kuelekea Uchaguzi wa AMANI.

Mapato ya Mechi hizo yatumike kusaidia Kambi za Watoto wenye asili ya Albinism pale Buhangija-Shinyanga na kwingineko kule ambako kuna kambi hizo.Lengo kuu la Mechi hiyo ni kuwaanda vijana kujua Uchaguzi si ugomvi bali ni nani apewe fursa na jamii husika kuchaguliwa kuongoza ngazi yoyote ile iwe ni Diwani, Mbunge, au Rais wa Nchi kutokana na jinsi muhusika alivyofanikiwa kushawishi Wananchi kuwachagua kwa mujibu wa vyama vyao.

Kama mechi hii itafanikiwa basi, inaweza kuuzwa kwa hisa za udhamini kwenye makampuni kama
1:Radio & TV Station:
Azam Television, IPP Media, Clouds Media, Star Media TV, Channel Ten,TBC,

2: Makampuni ya Simu
Vodacom, Airtel, Zantel, Tigo

3: Magazeti;

Washiriki wa hiari pia kama Wasanii wa Muziki wenye hamasa kwenye jamii bila kujali itikadi zao [Pro Jay, Afande Sele, Diamond, Jide, Juma Nature, Weusi, AY, Mwanafa, Ngosha Ze Don, Wanaume, Yamoto band, Roma Mkatoliki, na wengineo ambao wana haiba fulani kwenya jamii.

Na Stakeholders wa mechi hii wawe, Vyama vya Kisiasa husika ambavyo ni CCM, CDM, NCCR na CUF pia Tume ya Uchaguzi NEC, na PCCB.

Kupitia Wadhamini hao tume ya Uchaguzi na PCCB watapata Stage kuwaanda Watanzania kupitia Meseji mahususi kuona uchaguzi kama sehemu ya mchakato muhimu wa kupata viongozi Bora kupitia vyama shiriki.

Niwazo tuu.........kumuona kitu Sugu inapasha............mbele yake kitu Dongo Janjalooo inapasha........eeehehee pande ya pili kuna kitu Riz moko nayo inapasha, ikifuatiwa na Lusinde mambo ya kibajaji...

Kwa sie tusio na vyama tunaona umuhimu wa mechi kama hizi uwaanda Vijana kisaikolojia kwa mapokea na mihemuko...kwa kuwa uwa tunajua maumibu wanayoyapata Yanga wakifungwa na Simba au Vice versa pia.Lakini kwa kufungwa huko ligi ya Soka Tanzania uendelea na Maisha ya Watanzania uendelea kama kawaida pamoja na tofauti kubwa na kali za mapenzi ya Timu husika kwa kila mmoja wao iwe SIMBA ama YANGA.

Nasubilia kipute hicho..........uwanja wa TAIFA....patakuwa HAPATOSHI....kama naiona vile....nyomi ya kufa mtu...Tuanzieee hapo.............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…