Msolo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2008
- 2,713
- 3,559
Imeandikwa na Dominick Salamba
https://www.instagram.com/dominicksalamba/
Kwanza kabisa natoa pongezi zangu za dhati kwa Timu ya Taifa kwa kuonesha ukomavu katika fainal za mataifa ya Afrika hasa nimpongeze kocha kwa kazi nzuri aliyofanya ingawa wengi hawaoni, na hapo ndipo inapokuja tofauti ya Kocha na mashabiki.
Sio kila timu inayofungwa basi lawama kwa kocha au benchi la ufundi kwani kinachoonekana uwanjani ni mjumuiko wa mambo mengi yaliyofanyika nje ya uwanja.. Kila nikiangalia timu yetu naona wamemaliza mambo yote kwa maana uwezo wa wachezaji ulifika mwisho, mbinu za mwalimu zilifikia mwisho kwa maana uwezo wa wachezaji kupokea na kutafsiri zilifikia mwisho na hata maarifa binafsi walimaliza sasa, ingekua ngumu kutoa kitu ambacho hakipo.
Sio kila kushindwa ni sababu ya za wanaoshindana kuna mda zinakua ni sababu za waliopelekea washindani kushindana..Leo tunawezaje kulaumu kocha kiasi cha kutaka aondolewe kwa jitihada zipi za wazi tulizofanya kama Taifa kwa maana ya wenye mpira, vilabu, baraza la michezo na wadau?
Tunataka kujifariji kwa kile walichofanya Misri jana baada ya kutupwa nje ya michuano au Uganda bila kuangalia mfumo mzima wa soka na uwekezaji uliopo katika hizo nchi na mwishoe tunataka kudandia gari kwa mbele kitu ambacho si sawa na hakiwezi kutufikisha..
Kila wakati tunapenda kufunika mambo kutokana na uhitaji wa vitu vya mkato mkato na kutaka matunda ambayo hatukuyaanda nani asiyekua mpira ni mchakato na si tukio?ziko wapi ligi za vijana?yapo wapi mafunzo ya ukocha ya soka la vijana? viko wapi vikosi vya timu b vilivyo imara vya timu za ligi kuu?, achana na hivi vingi vya kuungaunga? vikowapi viwanja bora vya soka vilivyotimia na vile vya soka la vijana,pamoja vile viwanja vya ndani ?upo wapi mpango mkakati wa Taifa juu ya maendeleo ya soka letu?
Baada ya kujibu yote hayo kwa vitendo hapo ndipo tutakua na uhalali wa kuhoji zaidi uwezo wa kocha ni sawa na kumlaumu kiziwi kwanini asikii wakati wewe umemwita kwa sauti kubwa.. Tuache mihemko kama hatukua tayari kuwekeza na kusubiri hata aje nani stori itakua ile ile,wamepita makocha wangapi kipi kipya tumepata?zaidi ya kuwatafutia sababu na kuwatimua?
Povu kawaida povukaa..#bakinasisi__