Kemby
Member
- Oct 5, 2013
- 28
- 14
Habari za Leo wana Jamvi, mimi ni mwanaume, nna miaka 26, kwa sasa nafanya kazi Kibaha, ingawa makazi yangu ni Dar. Sijawahi kuwa na historia ndefu ya kimapenzi, maana tangu nipo shule nilimpenda msichana mmoja tu na tukawekeana ahadi kibao za kuishi pamoja hapo baadae.
Kwa bahati miaka miwili iliyopita nilipata bahati ya kuanza kuanza kazi nje ya mkoa, nilimwahidi mpenzi kwamba anivumilie ili nikirudi tukamilishe mipango yetu ya ndoa. Nikiwa huko nilikuwa nawasiliana nae kipindi cha mwanzoni, lakini baadae kukawa na ukimya kidogo, sikujali sana kwani baada ya hapo tulikuwa na mawasiliano kama kawaida.
Nilipopata bahati ya ya kuja likizo huku baada ya mwaka nikafika maaneo ya nyumbani nikaanza kuskia habari ya kwamba mpenzi wangu kaolewa na amezalishwa, sikuamini nikaanza kutafuta hewani na kuomba kuonana nae maana wao walihama maeneo yetu.
Alinipiga chenga za hapa na pale, lakini niliamua kwenda maeneo yao kuuliza, nikafanikiwa kuujua ukweli. Jambo hili limeniumiza sana, nna miezi 6 sasa sina mpenzi wala mawasiliano ya karibu na mwanamke, ingawa sidhan kama atapatikana msichana wa kunielewa ila nna imani yupo msichana ambaye naye ana yake yaliyomsibu na muda umefika sasa wa ku settle down.
Mimi nafanya kazi, nna maisha yangu, regardless wewe upoje, tafadhali tuwasiliane, tufahamiane, nieleze yako, pengine tunaweza kuwa kama marafiki mwanzoni na hatimaye mambo yakabadilika, kiukweli nipo mpweke mno na ntapoteza mwelekeo.
Umri haujaenda sana ila kwa haya machache niliyoyapata nna hitaji kuwa na mwenza ambaye tutashauriana na kushirikiana katika mengi. kama unahisi umeguswa kwa uchache na haya, tafadhali, ni PM au Uliza tu hapa hapa.