Natamani kuwa fundi wa kutatua changamoto za magari, lakini sijui sehemu ya kuanzia

Natamani kuwa fundi wa kutatua changamoto za magari, lakini sijui sehemu ya kuanzia

ngorombo

Member
Joined
Jun 7, 2019
Posts
60
Reaction score
201
Habari wakubwa kwa wadogo. Awali ya yote nipende kumshukru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai, Maisha, pia zawadi ya kkutanishwa na watu mbalimbali, wenye mawazo mbalimbali, na mitazamo mbalimbali.

Kama kichwa cha thread kinavyo jieleza hapo juu.

Mimi nikijana niliye pata Elimu hadi kidato cha pili, mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Mbinga mjini. Kutokana na hali ngumu ya maisha nililazimika kusitisha masomo, kwasababu ya ya ukosefu wa vitu msingi katika safari hiyo ya kielimu.

Kusitisha kwangu kwa elimu ya secondary, ilikuwa ni wazo nzuri ,ambalo nilikuwa nimefikiria litanisaidia katika kutatuta changamoto binafsi;kama chakula, maradhi na mavazi bila kusahau.

Nipo mtaani kwa miaka miwili sasa, nikiwa na jishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile; saidia Ufundi ujenzi, kufanya vibarua kwenye mashamba ya watu, na shughuli zingine nyingi.

Kwa hiki kipindi cha miaka miwili nimeweza kupata kiasi kidogo cha pesa, ambacho kimenisaidai, pia nafikiri kitanikidhi katika baadhi ya mambo.

Nimekuwa nikifanya hizo shughuli kwa kipindi hicho chote, lakini sijawahi kuwa na furaha ya moyo. Dhairi, naona kuna kitu kimekosekana katika mimi. Hivyo, imenifanya nikafanya tafakari ya kina nika gundua itakuwa vizuri kama nikipata ujuzi wa kuwa fundi wa magari.

Kama nilivyotanguliza mwanzoni mwa uzi huu, ya kwamba jamii forum ni mahala sahihi, na watu sahihi, watakonisaidai kunipatia mwongozo au ushauri mwingine, wanini nifanye na vitu gani vinahitajika. Pia, kama kuna aina za huo ufundi.

Nimechagua ujuzi huo, kwasaababu nikitu nilikuwa nimekipenda toka nikiwa katika udogo wangu na ukubwa wangu. Nawaza kuwamwenye furaha kama nia na malengo yangu yatatimia.

Msaada wenu wa mawazo ni msingi wa mimi kuwa mimi, kwasababu bado sijawa mimi.

Kwa wale nitako wahudhi kwa mwandiko mchafu I'm very sorry in advance.
 
Nenda VETA miaka 3 ukitoka hapo upo vizur ila sasa utaangalia kwenye huo ufundi wa magari utachukua fani gani
Mechanics au ufundi wa umeme wa magari
 
Nenda hapo jimboni kuna chuo kizuri cha hiyo fani ya magari, fanyia utafiti vyuo kadhaa kama hicho, trade peramiho na veta. Ukiwa na cheti kutoka katika hivyo vyuo ukaongeza na udereva unakuwa na uwanja mpana wa ajira. Nakutakia mafanikio
 
Fika Ndanda hapo chuo cha Wajerumani ukitoka hapo we ni nyoko utakuwa utafutwa ulipo, nakushauri uchukue ufundi wa umeme wa magari, jikite zaidi kwenye kusolve kwa teknolojia achana na ufundi wa nyundo na bisibisi, all the best
Shukrani sana kwa mchango wako.
 
Nenda hapo jimboni kuna chuo kizuri cha hiyo fani ya magari, fanyia utafiti vyuo kadhaa kama hicho, trade peramiho na veta. Ukiwa na cheti kutoka katika hivyo vyuo ukaongeza na udereva unakuwa na uwanja mpana wa ajira. Nakutakia mafanikio
Asante sana
 
Back
Top Bottom