Natamani Misiba ya Wahaya iwe mingi kwani inatusaidia sana Kuimarisha Afya zetu kwa Vyakula na Kuoka Bajeti zetu za Kimaisha



Penda penda vya bure utakuja kubanduliwa siku moja.
 
Nakumbuka kwenye msiba mmoja kuna mzee mmoja alilia kwenye msiba tena mbele ya marehemu akidai sh 25 alizomkopesha marehemu mpaka alipewa hela ndipo akaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna dada mmoja nae mtani aliudhuria msiba wa dada mmoja alikufa wiki moja kabla ya harusi yake, yule mtani akaja na shela kuwa siku ile ndio siku ya harusi
 
Msamehe bure. Mimi nilipoanza kusoma nilijua ni utani.

Jamaa alisoma juu juu hakutaka kuumiza kichwa.

Sasa na wewe ndo umemuandama na matusi rasha rasha.

Ungemuelewesha tu taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Mi nataka wapare wadedi kwa wingi ili tubadilishe menu kwa kufakamia makande kwa wingi huku tukijifunza kubana matumizi kwa kugonga ugali kwa picha ya samaki perege.

Cc Mshana Jr , NAKWEDE
Haa ha ha ha, mkuu Asprin kumbe wewe ni MEKU!??? Haa ha ha ha, nimefurahi sana kaka kujua hilo
 
Haa ha ha ha, pole pole kaka, wengine bado wadogo hawajui haya; mimi nilipoona kichwa cha habari tu na mleta hicho kichwa ni wewe I knew it kwamba ndio mambo yale yale ya watu wa mkoani Mara na Kagera yameanza; kuna siku moja alikufa Mkurya Fulani mjeshi, wakati maiti inatolewa kwenda ayapoti kwa safari, Wahaya kadhaa wa hapa Dar walijioganizi na kuzuia jeneza lisitoke hadi wahakikishiwe eti ndugu yao ambaye ni marehemu atakunywa chai njiani, walisema hivi, "Hatuwezi kuruhusu maiti ya ndugu yetu itoke hivi hivi na kuanza safari wakati hatuna hakika kama atakunywa chai njiani, tunaomba kujua kama hela ya chai njiani kwa ajili ya ndugu yetu kama ipo" Ndugu wale Wakurya kama kawaida, walijichanga change haraka na kutoka na burungutu la pesa, na wao Wahaya wakatoa za kwao na safari ikaendelea, Watoto wadogo hawayajui haya mambo na ndio maana amekejeri bila kujua
 
Nakumbuka kwenye msiba mmoja kuna mzee mmoja alilia kwenye msiba tena mbele ya marehemu akidai sh 25 alizomkopesha marehemu mpaka alipewa hela ndipo akaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna Msiba mwingine ulitokea wa Watani zangu wengine Waha nakumbuka Watu wa Musoma ( Mara ) waliokuwepo pale Msibani walivizia Mwili umewasili na baada ya Shughuli zote za Kuuga ule Mwili kukamilika wakauzuia Kuondolewa hadi waende Kununuliwa pombe kali ya ' Gongo ' tena ya kutoka kwa Mama mmoja hivi ' Maarufu ' Tegeta ambapo kuna Watu walidhani Jamaa ( wana Mara ) hawakudhamiria ila huwezi amini aliitwa Dereva mmoja wa BodaBoda akapewa Hela na ramani inapouzwa na alienda haraka kuinunua na kurudi nayo kisha Watu wakainywa vile vile na baada ya hapo wakazuia Mwili usipelekwe na Gari hadi Makaburini na Wao ndiyo wakaubeba hadi Makaburini japo kulikuwa na Umbali lakini waliweza kubadilishana Jeneza hadi Makaburini.
 

Ha ha ha ha ha ha....Mkuu nimecheka sana. Halafu huwezi kuamini hao Watani wakikuambia hivyo au wakikupa hayo Masharti na usipoyafuata tegemea kuna balaa / nuksi fulani itawapateni ama hapo hapo au baada ya muda mfupi tu. Ukitaka kuwaweza Watani wakiyafanya yote hayo Wewe watii tu na kuwa mpole kwani hata wakikupiga ukienda Kuripoti Polisi wakijua mna Utani wa Kimila hata hao Polisi nao wanaweza Kukusindikiza na kukurudisha huko huko Msibani na ' Kipondo / Kipigo ' cha Kutukuka.
 
Tunataka mfe nyie wakurya..Ruge a.k.a kyoma tunamzika kwa ubabe j tatu wakurya na wajaluo mkija kwenye msiba was kyoma Ruge mtashinda njaa labda tuwape chupa moja moja ya lubusi basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mtani, ila mnabid na nyie mfe kwa wingi ili na sisi tujenge afya pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunataka mfe nyie wakurya..Ruge a.k.a kyoma tunamzika kwa ubabe j tatu wakurya na wajaluo mkija kwenye msiba was kyoma Ruge mtashinda njaa labda tuwape chupa moja moja ya lubusi basi

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu kuna Mhaya mmoja Msibani alikuwa ananiangalia kwa umakini mno huku pia akiniogopa na mara kwa mara alikuwa akiniuliza nataka Kula au Kunywa nini. Sijui alinishtukia kuwa labda Mimi ndiyo ' Mtani ' wake / wao GENTAMYCINE. Jamani Wahaya chelewesheni ' Kumzika ' Ruge kwani huu Msiba unaokoa sana ' Bajeti ' zetu za Kimaisha hapa mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…