Natamani mtoto, nifanyeje!?

miss nuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2014
Posts
513
Reaction score
191
Nina umri wa miaka 30, nimezaa mara mbili ila nina mtoto mmoja wa miaka 10, mwingine amefariki. Tatizo nililonalo ni kutopata ujauzito. Napata hedhi kwa mzunguko wa kawaida ila naweza nikaingia siku moja tu kwa mwezi halafu naanza kuona dalili za ujauzito kama kuvimba maziwa, moyo kwenda mbio lakini nikipima sioni mimba.

Nishaenda Hospitali nikaambiwa labda ni homon wakanipa dawa za baada ya muda nikapata mimba, siku niliyogundua nina mimba usiku wake tumbo likauma sana kufika asubuhi damu ikaanza kutoka nikaenda hospitali, wakasema ninywe amoxln nikanywa tumbo likapoa Lakini cha kushangaza baadae nilipopima mimba ikawa negative.

Dr nishauri nifanyeje, nina hamu ya mtoto.
 
Mkuu pole sana,najuwa the way unavyojisikia,kwa sababu na mimi ninatatizo kama hilo lakwako la kutopata ujauzito,ngoja wanaofahamu waje natumaini namimi nitajifunza kitu hapa,Mungu atausaidie.
 
Muone Dr. bingwa wa watoto.
 
Pole Miss Nuru.

Muhimu kumuuona daktari wakina mama na wafanye vipimo vyote kuangalia ni tatizo gani linasababisha upoteze mimba.

Wakigundua tatizo kuna uwezo wa kuzuia kupoteza mimba kwa kutumia hormones na uangalifu wa karibu sana wa daktari.

Gharama inaweza kuwa kubwa lakini kama unamtaka mtoto basi sidhani kama gharama itakuzuia.

Kila la kheri mwenyezi Mungu atakubariki.
 

Asante kwa ushaur nitaufanyia kaz
 
nimelia na Mimi Nina mtoto miaka 8 wapili akafariki 8 months na juzi mimba nimetoka ya miezi miwili
 
Kuna majani flani ya kipare, yanapatikana upareni, nasikia yanaweka kizazi sawa, ulizia wapare wanayajua
 


Kuna dawa inayotengenezwa kwa kirutubisho cha soya wasiliane. nao uweze kuipata ... Inatakiwa utumie dozi ya miezi mitatu

#+255714206306
 
sasa dada yangu si umeishaona kuwa kuna tatizo la homoni hapo? maana zaidi ya hapo labda tuseme kuna uvimbe ndani!!, hapo ulipats mimba na ikatoka sasa inabidi ijulikane ilitoka kwa sababu gani, bila shaka ni homoni husika kwa ajili ya kuikuza mimba zilikisekana, kwa vile umeishaonana na madaktari wa kawaida,ni muda sasa utafute specialist wa kinamama,kama unajiweza badi nenda hospitali za private(serikalini mlolongo mrefu).nena na kumbukumbu za awali na ujieleze vizuri, ikitokea ukapewa dawa bila kumuona mtaalamu basi we mtafute nesi yeyote mmama mzoefu,muekezw shida yako na umwombe akupe mawasiliano ya specialist husika.

kwa harakaharaka ni kwamba unatakiwa kuwa under special care kabla na baada ya mimba, maana kuna tatizo,mimba haitoki bure tu.

pia nakushauri uww unakuwa KACHUMBARI, weka na KABICHI MBICHI(cabbage) kila siku.tumia vyote vikiwa vibichi usipike.Ndani ya wiki mbili utaona mabadiliko makubwa,kama kuna uvimbe wowote kwenye mfuko wa uzazi basi utaisha wenyewe na maumivu kuisha, na mengine utashuhudia mwenyewe.
 
Uko wapi?tuwasiliane kama nikijua mahali ulipo itakuwa rahisi kukusaidia
 
Pia mwenge kwa mama Ngoma hospital kuna Dr kutoka china mtaalamu wa magonjwa ya wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…