Kwa ufupi Alizaliwa Fumbwe zanzibar,kipaji chake kilijidhihirisha pale alipokuwa anatembeza vyungu mitaani ambapo alikuwa anaimba kwa sauti nzuri sana na yenye pitch kubwa ya kike alipokuwa ananadi bidhaa zake baadae alisajiliwa Columbia Records(ambayo hivi karibuni ilisimamia kazi za wanamuziki kama Adele, Mariah Carey, celine Dion) ambapo alirekodi album yake ya kwanza kwa lugha ya kiswahili na kuwa msanii wa kwanza wa kike kuimba kwa lugha hiyo badala ya kiarabu kama ilivyozoeleka alitamba na nyimbo kama wewe paka,njia ugurusumbwe,uchungu wa mwana, nilikwenda matembezi pamoja na muhogo wa Jang'ombe na nyingine nyingi.