Natangaza rasmi dhamira ya kugombea Ubunge 2010


Tunasubiri tuone ilani ya chama chako kwanza!!!!!!!!!
 
safi sana mkuu, kazi kwa wakazi wa ubungo kumchagua huyu ndugu,

naomba mwaka huu tusikie upinzani nao wanapata jimbo dar sio ccm,
 
Hongera Mnyika.

Pengine safari hii ile jinx iliyoitawala jimbo la ubungo kupata wabunge wa hovyo litaondoka maana nahesabu toka wakati wa venance ngula, lamwai na baadae mzee keenja. Kijana huyu alikuwa kipenzi cha watu toka 2005 lakini sijui aliteleza wapi mpaka akshindwa lakini naamini maandalizi ya mapema safari hii yanaweza kumfikisha anapopahitaji.

La msingi ni kufahamu kwamba haya unayoyanzungumza sasa, hata kama kampeni hazijaanza ni ahadi na sisi wapiga kura tutaanza kukupima kuanzia na haya unayoyasema sasa kwa sababu hayo ndiyo yanayojenga ushawishi kwetu.

Kila la heri bro!
 
Du nilidhani unakwenda kugombea wewe kumbe unakwenda kumsupport mtu mwingine halafu unatuambia ili iweje?

- Ili uelewe kwamba wana-JF tutakutana huko kwenye uchaguzi wa taifa badala ya kukalia hapa tu, vipi kuna sheria imevunjwa au ni zile zile zako za Biodiesel?

FMEs!
 
Hongera Mnyika,
Usikate tamaa, tunahitaji vijana wengi zaidi kwenye Siasa maana watakuwa ndiyo wazee wetu wa hekima miaka ijayo
 
Tunasubiri tuone ilani ya chama chako kwanza!!!!!!!!!

Kujiandikisha NA KUPIGA KURA NDIO MUHIMU....kumuunga mkono humu pekee haisaidii...minority wantuchagulia viongozi Tanzania juat because wanapewa vitambulishi sasa watu walio kwenye ajira wankiona hicho kitambulisho hakina maana vile wanavyo vya kazi...
 
Logically, wewe ndiye uliyekuwa mbunge wetu hapo Ubungo, tunapata faraja mpya kwamba unagombea tena - Tunahitaji vijana wenye upeo wa kuona mbali na kuchambua mambo kama wewe - tungefanikiwa kuwa na vijana walau 50 tu wenye upeo kama wako basi Tanzania ingekuwa na hazima kubwa sana, - tunahitaji mchango wako bungeni - nakuombea mkuu uende ukawaongezee nguvu kila Dr.Slaa.
 
Mnyika,

1. Nini msimamo wako kuhusu Tanzania kuwemo kwenye EAC, na 'soko la pamoja'.

2. Pana udaku kwamba ulipewa 'michuzi/rujua/ulua/bakshish/takrima/kitu kidogo' ili matokeo ya uchaguzi wa mwaka ulee yaende kwa mpinzani wako, akikuahidi kwamba 'atakuachia na kukupigia debe' mwaka huu. Wasemaje?


Mlenge
 
Kila la kheri mkuu. I hop this time mejipanga vizuri kudhibiti wizi wa kura uliofanyiwa last time.
 
Hongera Mnyika kwa uamuzi wako.
Kila la kheri kijana mwenzetu naamini safari hii lazima kieleweke.
 
Tunakutakia safari njema yenye mafanikio, Ushauri, Wabongo hawana wito wa kupiga kura imiza weendi kujiandikisha na hatimaye wakupigie
 
This is what I call heroism!! Usitishiwe nyau Mnyika.

But Naomba usiwe kama yule mbunge mwingine kijana aliingia Bungeni na moto mkali, sasa hivi kimyaa!!

Tunatarajia utatuwakilisha vyema wana Ubungo na Watanzania wote kaka.

Asante
 
Hongera Mnyika na mafanikio mema kwenye mpambano.

Ila mbona kama unaongelea uchaguzi wa taifa wakati bado hujapita uchaguzi wa CHADEMA? Au huko CHADEMA vigogo mnapitishwa bila kupingwa?

Angalieni msije mkawapa CCM nafasi ya kuwaambieni CHADEMA ina wenyewe, hakikisheni taratibu zote zinafuatwa.

Pia angalia sana kura za huko vijijini maana vijana wengi wa hapo mjini ni wasanii tu na hawapigi kura.
 

Wewe FMES siasa sio ugomvi but nipo interested kujua unashabikia Chama Cha Mafisadi (CCM) au upinzani. Kimsingi sina imani na mwanaccm yeyote labda JKN angekuwa hai.

Mkuu Mnyika kaa chonjo na FMEs, hakuna udugu wala nini kwenye hili game, sijawahi kuona mtu anaplan kushindwa. Ni adui yako kisiasa huyu.

Asante na kila la kheri katika hii safari, usiogope wala kutishika na sauti ya umeme.
 
all the best katika safari ya ukombozi ...tunaamini unaweza
 
Mimi siamini baada ya kuangaika na kampeni mgombeya anaweza kuachia ubunge kirahisi hivyo.Kuna mambo matatu ya msingi ambayo atajiuliza
1. Mbunge kwa miaka mitano anapata kiasi gani?
2. Akifanikiwa kujijengea sifa kubwa jimboni anaweza kukubalia kuniacha?
3. Baada ya miaka mitano kuna uwezekano wa kutokushinda.
KILA LA HERI MNYIKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…