Natarajia kuwafungulia PSSSF kesi kwa kuninyima michango yangu

Natarajia kuwafungulia PSSSF kesi kwa kuninyima michango yangu

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Mimi nilikuwa mtumishi wa Halmashauri na nilistaafu kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha miaka 60.

Nilipofuatilia mafao yangu hawa wajamaa wakagoma kunilipa wakitoa sababu kuwa mpaka michango yote ambayo Halmashauri ilitakiwa inichangie zichangwe kwanza na Halmashauri husika kwenda PSSF ndipo wanilipe.

Mimi nikawaona hawa jamaa wa PSSF ni wakora sana. Mimi nikawaeleza kuwa mimi sitajali hata kama Halmashauri husika hawatachangia, wanilipe tu fedha zangu nilizochangiwa na Halmashauri husika hata kama ni kidogo bado wakagoma.

Sasa nawapa onyo la mwisho litakalowapata wasije wakanilaumu kwa kuwa fedha ni za kwangu na zilichagwa na Halmashauri na zipo kwenye akaunti yao.
 
Mimi nilikuwa mtumishi wa Halmashauri na nilistaafu kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha miaka 60. Nilipofuatilia mafao yangu hawa wajamaa wakagoma kunilipa wakitoa sababu...
Kuna kitu sikielewi maana mimi siko sekta rasmi. Hivi kwani kama mwajiri hakupeleka michango wao si ndio wanapaswa wakadeal naye?

Kumekuwa na hali ya kuwambia watu wanapoenda kudai michango yao eti waende wamwambie mwajiri apeleke michango yote wakati nachojua hii mifuko ina wajibu na nguvu kisheria ya kumchukulia ahtua wmajiri asiyeleta michango
 
Mimi nilikuwa mtumishi wa Halmashauri na nilistaafu kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha miaka 60. Nilipofuatilia mafao yangu hawa wajamaa wakagoma kunilipa wakitoa...
You are wasting your time.

Achana nao, utakuja kufa kwa presha ya moyo bure
 
Kuna kitu sikielewi maana mimi siko sekta rasmi. Hivi kwani kama mwajiri hakupeleka michango wao si ndio wanapaswa wakadeal naye? Kumekuwa na hali ya kuwambia watu wanapoenda kudai michango yao eti waende wamwambie mwajiri apeleke michango yote wakati nachojua hii mifuko ina wajibu na nguvu kisheria ya kumchukulia ahtua wmajiri asiyeleta michango
Nchi hii ina maumbwa wengi sana. Kazi ni Yao wanakwepa!
 
Hii ndio Tanganyika ninayoifahamu.

Nia na Malengo yao ukate tamaa uwaachie hizo fedha,ufe kwa msongo wa mawazo wategemezi na warithi wako wasote mpaka viatu viishe kwa kutembea wakifuatilia hizo fedha halafu wao wawanyime na kwenda kunywea juice.
 
Back
Top Bottom