Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Pamoja na sintofahamu ya maneno hayo ninayokutana nayo lakini hii sasa inapelekea kukosa umakini wa maneno hasa Kundi na Kikundi.
Kawaida kwenye vyombo vya habari hasa DW au BBC lugha ya Kiswahili husikia wakitamka Kundi la Taliban la huko Afghanistan.
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku Star TV nikasikia mtangazaji akisema Kikundi cha Taliban. Nikajiuliza hivi Taliban pamoja na kuchukua uongozi wa nchi ya Afghanistan bado ni Kikundi tu?
Labda mie sielewi tofauti ya maneno haya, naomba msaada.