Nategemea kuiona Southampton ile ile, sura mpya miguu ya zamani

Nategemea kuiona Southampton ile ile, sura mpya miguu ya zamani

Danpol

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
5,727
Reaction score
8,918
Southampton imeripotiwa kupokea zaidi ya $ 150,000,000 katika mauzo ya wachezaji wa 5 katika dirisha la usajili lilofungwa juzi (karibu $ 85,000,000 zikipatikana kutoka kwa mauzo ya Lallana na Shaw peke yake).

Kwa timu iliyopanda daraja misimu minne tu iliyopita kuipata nafas/bahati ya kuingiza $150M katika dirisha moja tu la usajili wasingeweza kuikata hata kidogo, iliripotiwa kua kulikua na hasira kutoka kwa mashabiki wao na baadhi ya wachezaji (hasa Morgan Schneiderlin) kuhusu timu yao kuuza wachezaji nyota, lakini mwenyekiti Ralph Krueger na meneja Ronald Koeman hawakutishika, ile ilikua nafasi muhimu kwa watakatifu kutengeneza uchumi imara wa club waliamua liwalo na liwe wakafanya biashara.

Timu inapofanya mauzo ya wachezaji wa 5 muhimu ndani ya dirisha moja uwezokano wa kufanya vibaya msimu unaofuata ni mkubwa mno kuliko kufanya vizuri, lakini hali ni tofauti kidogo kwa Sotoni, wameuza karibia nusu ya kikosi cha kwanza [ Rickie Lambert, Luke Shaw, Adam Lallana, Dejan Lovren, na Calum Chambers] the Saints did an outstanding job kuwekeza fedha walizopata kwa kununua wachezaji wengine

Baada ya veterani Lambert kuondoka watakatifu waliziba nafasi yake kwa kuwasajili Shane Long na Graziano Pellè. Shane Long raia wa Ireland kutoka Hull City kwa ada ya uhamisho £19.9 msimu ulioisha alifunga jumla ya goli 15 akiwa na Hull city , Graziano Pellè kutoka Feyenoord akiwa na record nzuri sana ya ufungaji wa magoli, magoli 50 kwenye michezo 57

Kuwapoteza Shaw na Chambers kwa wakati mmoja kwa kias flani ni pigo, Nathaniel Clyne (23yrs) raia wa uingereza aliewasili kwa watakatifu 2012 akitokea Crystal ni kipaji kingine katika beki ya kulia ya watakatifu, Ryan Bertrand aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Chelesea (left back) kwa pamoja ( Ryan na Clyne) wanategemewa kuziba nafasi zilizo achwa na Shaw & chambers

Usajili wa Dušan Tadić ($17.7m) kutoka FC Twente na Toby Alderweireld kwa mkopo kutoka Atletico Madrid huenda ukawa usajili bora wa msimu wa Sotoni, Tadić perfect replacement wa Adam lallana, Alderweireld " Belgium international " zao la Ajax kabla ya kujiunga na ATM, " versatile defender " ana uwezo wa kucheza CB&LB

Hawakuishia hapo, pia walisajili golikipa Forster CB;DM Florin Gardos pamoja na Sadio Mané waliogharimu jumla $45.2 m kwa pamoja, Mané raia wa senegal ( 22yrs) alisajiliwa siku ya mwisho, ni kiungo/winger ameifungia timu yake ya zaman( Red Bull Salzbur) jumla ya goli 45 kwenye michezo 87

Wakati wengi wakiamin itashuka daraja, mie nakataa, kuna uwekekano mkubwa sana wakamaliza ndani ya top 10, walifanikiwa kuwabakisha Schneiderlin, Victor Wanyama, na Jay Rodriguez, wameleta maingizo mapya ambayo mengine ni bora kuliko ya walioondoka, Kazi imebaki kwa kocha na wachezaji

by Dan Pol
 
Yanga na simba uza wachezaji watano kwa msimu uone! Utajifungia ndani msimu mzima
 
Soton na BvB ni timu lizizoadhiriwa na hii tabia mbaya ya vilabu vikubwa kuchukuwa wachezaji wa timu zilizojijenga tayari kutoa upinzani wa kweli.

Ki ukweli Soton msimu uliisha ni moja ya timu zilizocheza mpira mzuri bila kujali matoke yalikuwaje. Wameporwa Lambert, Lorven, lalana, chambers na luka Shaw. Hivyo hivyo kwa dortmund wamewanyanganya Levy, Gotze, Nuer na wengine.
 
Soton na BvB ni timu lizizoadhiriwa na hii tabia mbaya ya vilabu vikubwa kuchukuwa wachezaji wa timu zilizojijenga tayari kutoa upinzani wa kweli.

Ki ukweli Soton msimu uliisha ni moja ya timu zilizocheza mpira mzuri bila kujali matoke yalikuwaje. Wameporwa Lambert, Lorven, lalana, chambers na luka Shaw. Hivyo hivyo kwa dortmund wamewanyanganya Levy, Gotze, Nuer na wengine.

Neur alikua Schalke 04
 
Naona wanaeoekea mule mule
 
Back
Top Bottom