OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Katika utafiti nilioufanya kwa kutumia data za kuanzia 2010 hadi 2020( Monthly) nikitumia VECM model, zimeonesha deni la taifa linaiweka nchi katika hali ya kuingiza Economic Shocks kutoka nje ya nchi ambayo huathiri utekelezaji wa sera ya fedha. Aidha, Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imeziandika Global Prices kama moja ya changamoto za utekelezaji wa sera ya fedha.
Global Prices ni kama bei za mafuta nk. PIa manunuzi kwa kutumia fedha taslim yalitajwa kuwa ni changamoto ambapo suala hilo lilisemwa na Prof. Luoga alipokuwa akizindua Benk Kuu kanda ya ZIwa
Kwa deni la serikali, kukopa nje kulileta economic shocks, wakati wakikopa ndani husabababisha sekta binafsi zikope nje kwa kuwa benki hukosa fedha za kuwakopesha. Ili kuepuka suala hilo, la serikali kuacha kukopa na watu binafsi kupunguza kiwango cha kukopa nje, nimeshauri kutumia 'Fiscal means' ili kudhibiti uchumi bila kuathiri masoko ya fedha na kuipa nguvu sera ya fedha.
Siwezi kushauri suala la tozo za miamala, kwa kuwa ninapaswa kuanza kulitafiti tatizo hilo kabla sijalizungumzia kuona athari zake za muda mrefu lakini kwa sasa nasema haya
Serikali imesema inatoza kodi ya uzalendo ili kujenga miundombinu, hivyo natarajia Deni la serikali litapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tumeanza kutumia fiscal means kupata fedha za ku-finance miradi. Kama lengo hili halitatimia ndani ya mwaka mmoja nitalazimika kuhoji kwa kuangalia miradi ambayo itakuwa imeshatekelezwa hadi wakati huo
Kifupi ni kuwa, tozo zinagharamia miradi, awali tulikuwa tunakopa kugharamia miradi, sasa kwa kuwa tozo inagharamia miradi husika ni lazima tuone 'significant' change kwenye deni la serikali
Signed
Economist, Researcher. OEDIPUS