Nateseka mwenzenu msaada pliz!

menny terry

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
509
Reaction score
670
Nimekuwa nikiumwa na kichwa sana.nilipima na kukutwa na malaria nikatumia metachelphin alafu nikachoma sindano aina ya antmethor.lakin hakija tulia nikaenda kupima typhoid nikakutwa nayo nikaamua kutumia dawa za typhoid but still bado kichwa kinauma mbaya yaani kama sina dicloper pembeni ni balaa.Pia nimekuwa nikipatwa na maumivi kidogo kwenye uume wakati wa haja ndogo na muwasho hivi.nimetumia dawa za U.T.I lakini bado.kiukweli nateseka mwenzenu naombeni msaada wa ushauri .
 
Sikia kengele tulia na wako
<br />
<br /> Hapana mkuu mi sio mhuni nimeoa na ni na watoto wa wili beleive me or not .sija wahi toka nje ya ndoa hata mara moja.
 
pole sana rudi tena hospital, ila metakelfin siku hizi haishauriwi sana
wanasema ukishindwa dawa mseto tumia duo-cotexin ni dawa nzuri kwa
malaria.
 
pole sana rudi tena hospital, ila metakelfin siku hizi haishauriwi sana
wanasema ukishindwa dawa mseto tumia duo-cotexin ni dawa nzuri kwa
malaria.

Jeji kakushauri vizuri sana. dawa ya Metakelfin ilishasimamishwa kutuika kutibu malaria kwani vijidudu vya malaria vilionyesha usugu kwa kiasi kikubwa sana dhidi ya Metakelfin. Tatizo ni kuwa dawa hii unatumia vidonge vichache na kwa mara moja tu kwa hiyo watu wengi wanaipenda.

Dawa zinazotumika sasa kwa kutibu malaria ambazo hazina usugu mpaka sasa ni dawa za mseto, zipo nyingi ikiwemo pia DuoCotexin (my personal favourite), Coartem (ALu), Artequine (hii watu wengi wanalalamika inachosha), etc.

Uliporudi hospitali walikucheck Typhoid na kukupa pia dawa za UTI, lakini hawakurudia kucheck malaria kuona kama imeisha au la..nakushauri urudi kwa daktari kwa uchunguzi lakini pia waombe wakucheck tena malaria..
 
Hapo mkuu itakuwa ni malaria tu na hakuna tatizo jingine,Riwa amekushauri vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…