Katika kusaidiana kupata msaada wa Mungu,mimi nina jambo ninalolifahamu ambalo ningependa kukupa naamini linasaidia sana,ni very powerful weapon katika vita hizi.
Nalo ni moja tu...JINA LA MWENYEZI MUNGU.
Jaribu kila usalipo utamke Jina halisi la Mwenyezi Mungu kumuomba msaada.
Na uwe unarudiarudia sala hiyo(iwe fupi) mara kwa mara hata utembeapo,uwapo ofisini etc.
Sijui wewe ni dini gani,ila mimi nafahamu Jina la YAHWEH mkuu,Muumba mbingu na nchi.
Sisi wakristo tunapomaliza kusali huwa tunasema KWA JINA LA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
Sasa hapo mimi hutamka majina halisi,yaani YAHWEH,YAHSHUA na RUACH ELOHIM.
YAHWEH ni Jina kuu la Mwenyezi Mungu,maana yake MIMI NIKO(and bring everything into existence).Halafu YAHSHUA(YESU) maana yake ni YAHWEH NINAYEOKOA na RUACH ELOHIM maana yake ni Roho/pumzi/upepo wa Mungu wenye nguvu na uelekeo according to his purpose.
Ni upepo huu hutumika kupuliza pumzi ya uhai ambayo Mungu humpa kila mtu anapozaliwa.Ile pumzi inakuwa kama signature,yaani kusudi la Mungu juu ya mtu au kiumbe huyo,kusudio lake la kupewa uhai,kusudi hilo ndio wanajimu na wachawi huita nyota ya mtu.
Sasa hebu tafsiri hili unakuwa unamuita Mungu anayeishi(aliyepo),ambaye amekufanya uwepo,na anaweza kukutendea neno unalomuomba akalifanya likatokea(likawepo),akuokoe kwa kutumia nguvu yake ya kiungu (roho) ije kutenda kile ulichoomba but according to his will.(Huu upepo/Roho ndio tool ambayo Mungu anaitumia kufanya analotaka liwepo likawepo its a certain divine power,force.)
Matamshi haya pekee tayari ni mkataba kati yako na Mungu na sala itakayofuatia lazima itende kazi katika maisha yako kwa namna ya kipekee sana.Nazungumza kitu nilichokiexperience in real life.
Angalizo tu,huwezi kufikia kumuita Mungu kwa kiwango hiki halafu usiwe serious na ulichoomba.Ni jambo lenye uwajibikaji ndani yake.Imeandikwa Kila alitajaye Jina la Mungu na auache uovu.Na pia imeandikwa "Usilitaje BURE jina la Mungu".
Kama umeamua kufikia hatua hii basi uwe na shida yenye uzito wa kufanya hivyo, uwe rohoni umeamua kwa dhati ndipo umuite Mungu kwa staili hii.Vyovyote iwavyo majibu utayapata.Kama uko serious utapata majibu na pia kama hauko serious utayapata majibu yatakayokufanya uwe serious!
Sometimes tukiwa tumeelemewa sana hatuwezi hata kujiamini kutunga sala ili umfikishie Muumba wako.
Kama uko katika hali hiyo,unaweza tu kuchukua biblia,tafuta kitabu cha Zaburi,Soma Zaburi sura ya 10;1-17 kwa ajili ya kupambana vita na roho yoyote chafu.Unaposoma Zaburi hii kila penye neno BWANA sema "El Meez" maana yake "Mungu mtetezi wa wanyonge" na moyoni mwako ukimwona hivyo.Ukimaliza mwambie El Meez nisaidie mimi fulani mwana wa..(tamka jina la kwanza la mama yako).
Atakuja Ruach Elohim kukusaidia kwa nia ya Yahweh akiwa kama El Meez msaada wako.
Zaburi hii ya "kivita" iendane na Zaburi za toba (Zaburi 6 na Zaburi 25).Unaweza usiku kusoma zaburi hizi za toba na asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako unasoma ile ya mapambano.Ufanye hivyo mpaka pale utakapoona nafsini mwako kwamba umeomba vya kutosha kilichobaki ni Mungu mwenyewe kujibu,then switch to Zaburi sura ya 8.Ni ya kushukuru,kusifu na kuabudu na kutambua mamlaka ya kibinadamu ambayo Mungu amekupa juu ya nchi na hakuna wa kukuondolea mamlaka hiyo.
Unairudisha mamlaka yako na akili zako kwa Muumba wako na wewe mwenyewe,badala ya kuhofu na kuwaza viumbe wengine walioumbwa kama wewe tu,na hawana cha kukufanya ukisimama na Mungu wako.
God bless you,na ushinde,ukaishi kwa Jina lake.