National Board of Accountants and Auditors Tanzania (NBAA) Tanzania kila muda ukiisha huchelewa kuteuliwa nyingine

National Board of Accountants and Auditors Tanzania (NBAA) Tanzania kila muda ukiisha huchelewa kuteuliwa nyingine

Mulyambange

Member
Joined
Mar 14, 2015
Posts
62
Reaction score
20
National Board of Accountants and Auditors Tanzania ina bodi ambayo huteuliwa na Rais wa Nchi. Kwa bahati mbaya sana imekuwa kawaida sasa kila ikimaliza muda huchelewa kuteuliwa nyingne na hiii imekuwa ikichelewesha kutolewa kwa matokeo yake ya mitihani husika. Kwa mfano mwaka 2017 na 2018 Bodi haikuteuliwa kwa wakati ilipelekea matokeo kuchelewa kutoka.

Hivi sasa matokeo May 2021 hayajatangazwa kwani Bodi iliyopo imemaliza muda wake na haijateuliwa nyingne so matokeo hayawezi tangazwa mpaka kuwepo bodi.

Huenda management ya NBAA haipo makini kutarifu mamlaka za uteuzi juu ya hili. Pia huenda management imefanya yake kutoa taarifa hivyo mama hajapewa faili husika mpaka sasa.

MAOMBI KWA WAHUSIKA
Timizeni wajibu wenu mnaumiza wahasibu na wakaguzi watarajiwe kwa kushindwa kufanya usajili wake.

Pia chama cha wahasibu Tanzania [emoji1241] hii ni moja ya kazi ambazo zinagusa masirahi ya wanachama wenu.

Mbona mpo kimya?
 
Back
Top Bottom