NBAA itashindwa kuandaa mitihani kwaajili ya wanafunzi wanaosomea uhasibu ifikapo Julai 2018 kama wajumbe wa bodi yake ya uongozi hawatakuwa wameteuliwa na waziri mwenye dhamana.
Kwa namna isiyo ya kawaida, majibu ya wanafunzi wa uhasibu waliofanya mitihani yao mwezi Novemba 2017 hayakuweza kutoka kutokana na kukosekana kwa bodi ya uongozi ambayo ilikuwa imekwisha muda wake tangu mwezi Septemba 2017. (Mwenyekiti wa bodi hii huteuliwa na Raisi, na wajumbe huteuliwa na Waziri wa fedha)
Kwa mujibu wa taratibu za NBAA, bodi hii ndio yenye uwezo wa kupitisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi.
Kitendo hicho kilisababisha taharuki na mshangao kwa wasomi hawa ambao hawakudhani hata sikumoja kama kitu kama hicho kinaweza kutokea.
“Sidhani kama unaweza kusikia kitu kama hiki kwenye mitihani ya ACCA” alisema mwanafunzi mmoja kwa malalamiko.
Bodi ya wadhamini iliisha muda wake mwezi mwezi wa Septemba mwaka 2017. Kwahiyo alitakiwa ateuliwe mwenyekiti wa bodi mpya na wajumbe wa bodi mpya mapema ili majibu ya mtihani wa Novemba yaweze kutoka kuanzia japo tarehe 20 Disemba 2017 mpaka 24 Disemba 2017 kama ilivyokuwa kawaida miaka ya nyuma. Uteuzi haukufanyika, na hivyo matokeo hayakutoka, na wanafunzi wakabaki wamepigwa na butwaa.
Baada ya matokeo, wanafunzi wanakuwa wakijua kama wajiandae na mitihani ya masomo gani tena. Kwasababu mitihani waliyofaulu wanaachana nayo na kusoma ambayo bado hawajafaulu au masomo ambayo hawajawahi kufanya.
Kwahiyo madarasa yakaanza January 2018 wakati majibu hayajatoka.
NBAA ikatoa muongozo kwamba mwanafunzi hataruhusiwa kufanya mitihani ya masomo ambayo majibu yake bado hayajatoka.
Sasa kwa wanafunzi ambao walikuwa bado wana mitihani hawajawahi kufanya, ikawa ni rahisi kwao, wakajiandikisha kufanya hiyo mitihani mipya.
Lakini kwa wanafunzi ambao walikuwa wamemaliza mitihani yote, na hawana mitihani mingine ya kufanya zaidi ya kusubiri majibu hayo ndio wajue nini cha kufanya, ikawa hawajui wafanyaje zaidi ya kuchanganyikiwa.
Mitihani ya wanafunzi waliokuwa wanaanza maandalizi yao Januari 2018 ilitakiwa kufanyika Mei 2018. Matarajio ya wanafunzi wengi ilikuwa ni kwamba ifikapo kipindi cha mitihani majibu ya mitihani iliyopita (yaani November 2017) yatakuwa yameshatoka.
Wiki tatu kabla ya mitihani (11 Aprili) ukatangazwa uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya uhasibu. Kitendo hicho kilitakiwa kifuatiwa na uteuzi wa wajumbe wa bodi. Matarajio yakawa kwamba mambo haya ngefanyika haraka na kuwawezesha wanafunzi wa uhasibu wasiokuwa na majibu kuyapata haraka, ili waliokuwa tayari kufanya mitihani ya mwezi Mei wafanye hivyo. La hasha! Wajumbe hawajateuliwa hadi leo hii ninapoandika uzi huu.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema NBAA wamejaribu kufuatilia kwa waziri mwenye mamlaka ya uteuzi kuhusu uteuzi wa wajumbe hao mpaka wamechoka na hakuna dalili za kuteuliwa wajumbe wa bodi hiyo haraka.
Kwa mujibu wa taratibu zao, hawataweza kuendelea tena na kutunga na kusimamia mitihani ifikapo Julai 2018 kwasababu watakuwa wamekiuka taratibu nyingi sana na haitawezeana tena.
Mheshimiwa Rais, ingilia swala hili mapema lisije likaendelea kututia aibu nchi na kusababisha matatizo kwenye taaluma hii ya uhasibu.
Muendelezo - 24-05-2018
Kuna habari za kuaminika kwamba jana tarehe 24 Mei 2018 majina ya wajumbe wa bodi ya uhasibu yameshateuliwa na kufikishwa kwenye bodi ya wahasibu.
Na huenda matokeo ya mtihani wa mwezi Novemba mwaka 2017 yakapitishwa na bodi na kutangazwa mwishoni mwa mwezi huu Mei.