-Ni wazi kwamba dunia nzima matumizi ya simujanja(smart phones) na kompyuta yametawala kwa kiasi kikubwa.
-Ni vyema kwa serikali kuanzisha mfumo utakaojulikana kama NATIONAL DIGITAL MARKETING (NDM) ambapo itakuwa ni teknolojia ya habari na mawasiliano katika nyanja ya biashara na masoko.
-Biashara nchini Tanzania katika sekta mbalimbali zimekuwa na mauzo madogo au kufanikiwa kwa asilimia chache kwasababu ya ugumu wa masoko(marketing).
Mfumo huu wa kitofauti wa serikali utaweza kurahisisha kabisa biashara nchini na mauzo kwa ujumla na kutatua changamoto ya ugumu wa masoko.
-Ni kweli kwamba Tanzania inazalisha bidhaa nyingi za kilimo,viwanda,madawa n.k
NDM itakuwa ni mfumo wa kisayansi zaidi ambao utaruhusu wafanyabiashara wa juu,kati,na chini kujisajili(kujihusisha nao).Mfumo utaainisha bidhaa zinazouzwa,muuzaji,mahali,ubora na gharama za bidhaa
Ama wanunuzi watumiaji au wanunuzi wauzaji watajisajili na kuainisha bidhaa wanazo hitaji na mfumo utaonyesha mwisho(limit) wa muda wa uhitaji wa bidhaa kwa mteja.
-Mfumo wa NDM utaruhusu biashara za aina mbili (biashara za ndani na biashara za nje ya nchi).
Biashara za ndani ya nchi zitajumuisha marketing na mauzo ndani ya nchi tu kama itakavyoonekana katika picha...
Ama kwa biashara za nje ya nchi pia wafanyabiashara wa nje watajisajili katika NDM ili kununua na kuuza bidhaa hizo kulingana na mahitaji ya wateja.
NDM ITATUMIKA VIPI?
-kwa kila atakayejisajili awe mfanya biashara mkubwa, wa kati au wa chini ataingia katika mfumo online na kujaza taarifa zake zote muhimu ikijumuisha na taarifa za bidhaa kama vle bei ,ubora mahali n.k
-Mfanyabiashara ataruhusiwa kutafuta wateja waliojisajili na kuwasiliana nao ili kuuza bidhaa zake.
-Ama kwa wanunuzi watumiaji au wanunuzi wauzaji na wao pia wataingia katika mfumo kujaza taarifa zote muhimu kama vile bidhaa anayoitaka,mwisho wa muda wa uhitaji wa bidhaa,idadi ya bidhaa n.k
-Ama kwa wanunuzi walio nje ya nchi wataingia katika mfumo wa NDM na kuagiza bidhaa za jumla au hata rejareja na kulipia jumla ya gharama ikihusisha gharama za usafiri kama vile basi au ndege.
-Bidhaa zote zitakazo husishwa katika mauzo ziwe za wananchi,watu binafsi na hata za serikali.
MFUMO WA NDM UTAZINGATIA YAFUATAYO
1) Mahitaji na matakwa ya wateja ili kutoa bidhaa zitakazowakidhi
2)Mfumo utasimamia bei kwa ufasaha,na kama bei itakuwa sio sahihi mfumo utagoma kuridhia(ku confirm) mauzo kwa bidhaa husika
3)Mfumo utakuwa na sehemu ya kuwasilisha mawazo(comments) moja kwa moja kwenda serikalini ili kukabili changamoto za wafanyabishara, wateja na hata changamoto za bidhaa.
4)NDM itakuwa na sheria zake binafsi ambazo zitawekwa na serikali kama vile
6) vyeti vya tuzo(certificates of awards) zitatolewa kwa wafanyabishara watakaonekana wameendelea na kukua kibiashara baada ya kutumia NDM.
SERIKALI NA TAIFA KWA UJUMLA WATAPATA FAIDA GANI
-Kwa biashara zote za juu,kati na chini na kwa wafanyabiashara wote waliojisajili, NDM itaweka kodi(tozo) tofautitofauti kulingana na maeneo ya biashara,aina ya biashara,ukubwa au udogo wa biashara.
- Mapato(tozo) italipwa kwa aliyejiandikisha katika NDM na atalipia kwa kila mwezi kama mfumo utakavyoonyesha wenyewe.
-Serikali itafatilia wafanyabishara na wateja wote ndani ya NDM na kuhakikisha tozo(kodi) imelipwa kwa asilimia zote
- Ongezeko la ajira litakuwa kwa kasi sana kadri biashara za ndani na nje ya nchi zitakavyozidi kurahisishwa kutokana na matumizi ya NDM na pia ajira zitapatikana serikalini kwa wafuatiliaji na watu wa kurekebisha mfumo kila itakapohitajika.
NAMNA GANI WATU WAHAMASISHWE ILI WATUMIE(WAJISAJILI)
1) Vyombo vya habari,viongozi wa serikali kama vile raisi wa nchi na mawaziri watahusika katika kuitangaza NDM nchi nzima na kuelezea faida au umuhimu wa kutumia mfumo huo.
2) Mabalozi wa Tanzania nchini mbalimbali wataitangaza NDM kwa wafanyabiashara na wanunuzi kutoka nje ili wajisajili na kutumia mfumo huo.
3) wataalamu wa masoko(marketing) ndani na nje ya nchi wahusike asilimia kubwa kutangaza na kuhamasisha watu kutumia NDM.
NDM IWE YA NAMNA GANI NA IUNDWE(CREATED) NA NANI
-Timu ya wataalamu wa telknolojia ya habari na mwasiliano na wataalamu wa masoko kutoka ndani na nje ya nchi wahusike katika kufanikisha hili .
mfumo huu unaweza ukawa katika namna mbili
1)Tovuti(website) ya NDM
2) App ( programu) katika simu au kompyuta
NDM ITAHUSIKA PIA NA WAFANYA BIASHARA WENYE SIMU NDOGO
-katika matumizi ya NDM wafanyabiashara wenye simu ndogo(sio simujanja) wataruhusiwa kujisajili katika mfumo lakini watapokea ujumbe(sms) kuhusu taarifa za bidhaa na wauzaji au taarifa za bidhaa na wanunuzi kwa wateja ambapo ili kuepusha kukera watu ,taarifa hizo zitarushwa kwa muda maalum kila wiki,huenda wakatumiwa kwa wiki mara 2 au mara 3 kwani wafanyabiashara hao wa simu ndogo watakuwa na line maalum za simu ambazo watazisajili kwaajili ya kutumia NDM tu.
-Taarifa(sms)hizo zitaainisha taarifa zote za muuzaji,mnunuzi,aina ya bidhaa na bei.
-Taarifa zitakazoingia kama ujumbe katika simu ndogo zitaleta bidhaa kulingana na aina za bidhaa ambazo mhusika alijisajili katika mfumo na ataruhusiwa kufanya mabadiliko ya bidhaa wakati wowote.

- ulazima wa kutoa kodi(ushuru) kwani sheria ya ya mapato ya mwaka 2019 kifungu 332 haizingatii ipasavyo ukusanyaji wa mapato
- biashara zisajiliwe na mamlaka husika mfano BRELA
- Miamala ya kifedha ifanyikie mtandaoni au kwa cash n.k

Upvote
2