Hawa jirani zetu bwana wana mambo kweli kweli, Lugha rasmi inayotambulika hata kikatiba ni kiingereza, sasa hapo kwenye lugha rasmi nyingine ya pili ndo kasheshe linapokuja, miaka ya nyuma kabisa mfano wakati wa nduli Amin, kiswahili kilikuwa kikizungumzwa sana na utawala wa Amin ukakifanya kiswahili kuwa lugha rasmi pamoja na kiingereza, sasa baada ya kuondoka nduli watawala waliofuata wakakiondoa kiswahili na walitaka lugha ya Baganda au Luganda kuwa lugha rasmi pamoja na kiingereza kutokana na kwamba Kabila la Wa-baganda ndo wengi zaidi uganda (asilimia 18-19 ya waganda wote),basi ikaonekana kuwa lugha yao ndo rahisi zaidi kukieneza kwani tayari kina wazungumzaji wengi kuliko lugha za makabila mengine, sasa issue ikawa kwamba yale makabila mengine hasa yale ambayo si ya kibantu yanayopatikana maeneo ya kaskazini, kaskazini magharibi na mashariki ya Uganda hayakifagilii sana hicho ki-Luganda.., wao zaidi wanatumia kiswahili na kiingereza hivyo kiluganda bado ni nadra sana kukisikia kikizungumzwa maeneo hayo ila kwenye maeneo mengine ya Uganda kiluganda ndiyo lugha inayozungumzwa sana..
Hadi miaka ya hivi karibuni nadhani ilikuwa ni mwaka 2005 bunge la Uganda kwa shingo upande liliridhia kiswahili kuwa lugha rasmi tena baada ya kuona kwamba hakuna jinsi, kwa sababu kiswahili kimekuwa ni kama maji usipoyanywa, utaogea au utapikia..