Jem Lifesaver
New Member
- Jul 31, 2023
- 1
- 1
NPHI Card ni KADI ya kielectroniki inayotumia umeme na mtandao (Intermet data) lli mtu aweze kusoma/kuingia ndani ya kadi na kupata taarifa zilizopo ndani yake, utatengenezwa mfumo usioshikika kwa mkono (software program) ambao utakuwa unatumika katika matibabu ya mfumo na utasoma kadi za NPHI Card. Mtu atawekewa pasipoti yake ya tangu anazaliwa wakati wa kutengeneza kadi hii, ifikapo miaka mitano (5) atatakiwa kubadilisha pasipoti ya kadi.
NPHI Card ndani yake itakuwa na sehemu mbili ambazo ni;
a) Sehemu ya kwanza Itajumuisha taarifa za mtu ambazo hazihusishi afya, kama vile jina kamili, pasipoti, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, kabila, dini, makazi na Kazi anayofanya.
b) Na Sehemu ya pili itahusisha taarifa za ugonjwa, kama vile kitu gani kilimleta Kituo cha Afya, Kimemsumbua kwa muda gani, Alishawahi kulazwa, Kama jibu ni ndio, alifanyiwa vipimo gani, Baada ya kupimwa aligundulika anaumwa nini au ana talizo gani, Alitibiwa kwa dawa gani, Aina ya kituo alichotibiwa nakama ana ugonjwa wa kudumu au ugonjwa wa kurithi mfano PUMU, KIFUA KIKUU au SELIMUNDU.
Kadi hii itatengenezwa na kugharamikiwa na Serikali, Kama vile Chanjo za watoto zinavyogharamikiwa na Serikali. Pia hizi Kadi zitapatikana katika kila kituo cha kutolea Matibabu/Kituo cha Afya ambacho kimesajiliwa na Serikali.
Watu wote watatakiwa kupatiwa hizi Kadi zinazoitwa NPH card, isipokuwa wale watoto ambao wamezaliwa na kufariki hawatapewa kadi, ila wengine wote watafunguliwa Kadi na kupewa. Pia kwa wale wageni wanaotoka nje ya Nchi wao wanaweza kuomba kupatiwa Kadi au wanaweza kutumia Kadi zao za Matibabu wakatibiwa kama walivyozoea kutibiwa hapo awali.
KADI hii itatumika katika vituo vyote vya Afya vilivyosajiliwa kisheria na Serikali vinavyopatikana hapa Nchini Tanzania. Kwa maana hiyo kila Kituo ni lazima kuwa na Mfumo huu wa Kielektroniki ili kuweza kusoma taarifa za Mgonjwa kwenye Kadi. Na Mashine zitakaa sehemu ya Wagonjwa wa Nje 'OPD'- (Out Patient Department).
KADI hizi zitakuwa hazina uwezo wa kuhifadhi FEDHA, lla utaweza kuunganisha na Kadi nyingine za BIMA ya Afya kama vile NHIF, CHF, n.k.
Mgonjwa anapokuja kupatiwa Matibabu Kadi yake itabakia sehemu anapoanzia kujiandikisha Mahali ambapo ni Sehemu ya Wagonjwa wa Nje (OPD). Akishamaliza kupatiwa Matibabu ni lazima arudishiwe KADI, Hivyo anatakiwa apitie alikoanzia kujiandikisha ili Mhudumu atakaempa KADI aweze kuhakiki kama taarifa zake kama zimerekodiwa ndani ya KADI yake (Updated) kulingana na Matibabu aliyopewa ndipo achukue.
WASIMAMIZI
1. Kwa upande wa matumizi ya KADI hii, Serikali itaajiri watu amabao wamesomea kutunza kumbukumbu za Afya, ambao watahusika kuanzia Mwanzo wa Mgonjwa kufika hadi anapotoka katika Kituo cha Afya, Taarifa zake zitarekodiwa na kuboreshwa katika Mfumo na Kadi yake. Wakiwa wanasaidiana na mtu allyeajiriwa kwa upande wa Tehama.
2. KADI hii atakuwa anapewa mtu aitumie kwa miaka kadhaa na baadae atalazimika kuirejesha tena kufanyiwa Maboresho kama ilivyo kwa Kadi za Benki. Mfano ikawa baada ya Miaka Mitano (5) mtu atatakiwa kurudi Hospitali ili kuboresha taarifa zake kwa wale ambao Kipindi hicho chote HAWAJAUGUA au HAWAJATUMIA KADI hiyo ya Matibabu waliyopewa.
3. Endapo Mmiliki wa KADI hii ATAFARIKI, Familia yake itatakiwa kutoa taarifa kwenye Kituo cha Afya cha karibu ili waweze kumtoa kwenye MFUMO.
FAIDA AMBAZO ZITAPATIKANA ENDAPO MFUMO HUU UTATUMIKA
1. Itasaidia kupata Taarifa za Ugonjwa sahihi katika wakati muafaka kwa sababu kila wakati Taarifa zitakuwa zinaboreshwa katika mfumo.
2. Itasaidia kupata TAARIFA zilizosahihi na kuweza kuzitumia kwa ajili ya UTAFITI wenye Uhalisia.
3. Itasaidia kutambua kwa urahisi na kwa haraka endapo kama kuna Ugonjwa wa Mlipuko umeingia Nchini. Kwa Mfano, Kipindi cha Ugonjwa wa Korona Endepo tungekuwa tunatumia KADI hii, kila sehemu ya Kituo cha Afya Mganga Mkuu wa Wilaya angeingia kwenye Mfumo na angeweza kugundua Mapema kwa kuona watu wa sehemu tafautitofauti mbona wanasumbuliwa na dalili zinazofanana? angefanya utafiti/kufuatilia kwa wepesi nakupata jibu kwa haraka. Kwa maana hiyo hata kwa sasa ikitokea UGONJWA WA MLIPUKO ndani ya Nchi yetu ni rahisi kungundulika kwa Mganga Mkuu kwa sababu utaonekana tu kwa dalili za kufanana zisizokuwa za kawaida kuonekana kwa Wagonjwa wa sehemu tofautitofauti na Mganga Mkuu itamsaidia kufanya UTAFITI au kufuatilia kwa wepesi na atapata majibu kwa haraka na kwa urahisi kulingana na taarifa za KADI ya mgonjwa kuonekana kwenye Mfumo.
4. Itasaidia kwa upande wa Wahudumu wa Afya pindi wanaposoma Taarifa za ndani ya Kadi kujua kama Mgonjwa ni Wakudumu au yupo kwenye Dozi/anaendelea na dawa au laah. Hivyo Mhudumu ataweza kupata urahisi wa kujua wapi aanze kumsaidia Mgonjwa ili aokoe Maisha yake hata kama watakuwepo waliozidiwa na hawawezi kuongea, kwa wazee sana wasioweza kujieleza, wasioweza kuongea, wale waliokwisha wahi kupata matibabu nyuma halafu wakasahau, Wale ambao wana Maambukizi lakini hawataki kumueleza daktari, n.k, hao nao KADI zao zitamsaidia Mhudumu kupata taarifa zao na kuwatambua ili kuweza kuwasaidia wapate Matibabu kwa haraka zaidi.
5. Kupitia KADI hii itasaidia kupunguza Gharama kwa Mgonjwa na kurudia kupewa Matibabu aliyopewa kutoka Kituo kingine au kurudia kufanya vipimo ambavyo vilishafanyika, Hivyo wahudumu wataweza kujua waanze kupima vipimo gani vingine au wafanye kwausahihi zaidi na kubadili dawa.
6. Pia kwa kupitia KADI hii itawasaidia watu wa kitengo cha UKIMWI kujua idadi halisi ya watu wenye maambukizi ya UKIMWI na hawapo kwenye Dawa.
7. Itasaidia kujua ldadi ya watu wenye Ugonjwa Sugu na wanahudhuria kliniki kwa wanaotakiwa kuhudhuria kliniki kulingana na ugonjwa walionao au ambao wako kwenye Dawa za kila mwezi, kama asilimia inapanda ya ugonjwa na kwanini inapanda?
8. Pia itasaidia kujua VIFO vya watu kwa Ugonjwa upi kwa kupitia KADI wakati wa kutoa taarifa za Mgonjwa aliyefariki.
9. Mtu mwenye KADI hii anaruhusiwa kwenda kutibiwa muda wowote hospitali tofauti tofauti kama kadi ya NHIF nahaijarishi umetibiwa mara ngapi kwa siku.
Endapo Andiko likapita/kupitishwa basi serikali inatakiwa kuunda Kamati ya Wataalamu katika upande wa watu wa TEHAMA, Watu wa Takwimu (Health Informations), Madaktari katika Vitengo mbalimbali, Watu wenye uzoefu wa Bima,mfano watu wa kutoka NHIF (National Health Insurance Fund) na sehemu ambazo zitakuwa zimebaki za muhimu wataongezeka kwenye kamati hii.
Naomba kuwasilisha.

Upvote
2