NATO ni kundi la mbwamwitu wanaosaidiana kuua wale.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Bahati nzuri hakuna hakuna nyumbu anaemsadia mbwamwitu na Simba kuua nyumbu wenzake. Lakini bahati mbaya Kuna waafrika wanaoweza kusaidia wazungu kuua waafrika wenzake. Kuna watu wanaoweza kuzunguuka huko huko kuomba wazungu wainyime msaada nchi yake.

NATO ni kundi la nchi ambazo zinasaidiana kuua kitoweo na kula pamoja. Bahati mbaya vitoweo havina namna ya kujitetea mmojamoja au hata kwenye kundi. Kuna vitoweo ambavyo vinatumika kusaidia NATO kupata vitoweo vyao kabla ya wao wenyewe kugeizwa vitoweo pia.

Africa, Asia na Latin America ni vitoweo vya nchi za NATO hasa uingereza, ufaransa, ubelgiji, Italy, ujerumani, uholanzi, Spain, ureno na Marekani. Nchi hizi haziwezi kuishi bila kupora. Bahati mbaya viongozi wa Africa, Asia na Latin America wanajua lakini hawana cha kufanya juu la hili. Bahati mbaya zaidi nchi hizi zinasita pia kuwa nyuma ya Urusi, china na North Korea kujilinda dhidi ya NATO. Wanarambishwa pelemende (mikopo na misaada) na NATO ili kujitenga na Urusi, China na North Korea wakisubiri muda wao wa kugeuzwa kitoweo mmoja baada ya mwingine kwa nyakati tofauti. Yaani wao hawezi kuungana kumpinga NATO lakini pia hawezi kumuinga mkono waziwazi yule anaeweza kumpinga NATO (adui yao).

Nani katuroga?
 
ogopa mtu anayishi fikra za maisha 1000 mbeLe walijua inawezekana baada ya ukoloni wasipoweka allience imara pangechimbika
 
ogopa mtu anayishi fikra za maisha 1000 mbeLe walijua inawezekana baada ya ukoloni wasipoweka allience imara pangechimbika
Kama ukijanjaruka NATO itakupiga. Gadaff, Assad, sadam, Iran, Putin, walionekana wakwamishaji wa maslahi yao.
 
Kwa Putin wamekwama labda wazichange upya karata zao
 
Kwa Putin wamekwama labda wazichange upya karata zao
Nyumbu Wana bahati ya kuwa na dubu (Russia) kwenye kundi lao, kazi yao ingekuwa kutumia pembe na kwato zao kumsaidia dubu kumpiga mbweha (NATO), lakini cha ajabu baadhi ya nyumbu (Ruto) wako upande wa mbweha waziwazi kumpiga dubu. Eti Ruto nae anaungana na NATO kumlaani Putin kuivamia Ukraine.!!! Anacheza Ngoma asiyoijua au kwa kulazimishwa
 
For the world to become a better place to live, there must be a leader country, and that's the U.S and their European cousins..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…