Natoa huduma za usaidizi katika kuandika miradi na mawazo ya biashara

Natoa huduma za usaidizi katika kuandika miradi na mawazo ya biashara

The BornAgain

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2024
Posts
428
Reaction score
582
Habari,

Moja ya maeneo yangu ya ushauri na utendaji kama ushauri na usaidizi ni katika kuchanganua mawazo ya uanzishashwaji miradi ya kiuchumi na kijamii pia uendelezaji wake.

Na katika hayo nipo vema kwenye:
1) Uandishi wa maandiko ya miradi (sio copy/paste au edits), naandika baada ya kufanya study ya kutosha kwenye wazo lako au mradi wako. Itategemea lengo vile tutaongea ili tujue hitaji husika.

2) Ushauri na kutafuta external funds kwa ajili ya mradi wako, ila kumbuka lazima uwe na asilimia kadhaa ya kujichangia mwenyewe sio kukutafutia 100% financing.

3) Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mradi wako popote ulipo Tanzania ili kukupatia report yake na kukushauri kulingana na matokeo ya tathmini au study, kisha ujue mfano kama kuna haja ya kujiongeza zaidi, au kupunguza rasilimali, au kufunga mradi, nk

HII NI KWA AJILI YA WANAOAMINI USHAURI WA KITAALAMU NA ANADHANI ANAPUNGUKIWA WELEDI FULANI KTK MRADI AU BIASHARA YAKE.

Gharama ni kiasi kinachojadilika kwa kadri ya kazi tutayopeana. Na hata kama hufanyiwi basi fanya mwenyewe hayo juu kwani ni mhimu kwa uhai wa mradi wako
 
Hii ni kwa wale wanaohitaji uhakiki na uhariri wa kazi zao au maandiko yao, hasa kwenye eneo la mapendekezo ya mradi, michanganuo ya biashara, mapendekezo ya tafiti, au taarifa za maudhui yenye mwelekeo wa masuala ya kiuchumi na kijamii. Natoa huduma hizi ili kufanya kazi yako iwe ya uhakika katika maeneo ya usahihi wa lugha, mpangilio, na mtiririko wa mawazo yako. Nafanya hivyo kwa weledi na utulivu mkubwa.

Kwanini? Ni kweli unaweza kuwa mwandishi mzuri na mbobezi katika eneo lako, lakini ukimpa mtu mwingine mwenye weledi na uzoefu, anaweza kugundua mapungufu kadhaa ambayo hukuyagundua mwenyewe. Japokuwa inapendekezwa kila ukiandika kazi yako, hata kama ni barua, uirejee yote ili kugundua makosa madogo madogo, kumpa mtu mwingine kufanya uhakiki na uhariri kunaweza kuwa bora zaidi. Hatua hii ni muhimu sana, usipuuzie maana kosa dogo tu linaweza kukupotezea umahiri au kuharibu dhana yako.

Asante.
 
Back
Top Bottom