Natoa pendekezo matokeo ya kuanzia shule za msingi hadi A - LEVEL yawe kwa mfumo unatumika kwenye matokeo ya darasa la saba

Natoa pendekezo matokeo ya kuanzia shule za msingi hadi A - LEVEL yawe kwa mfumo unatumika kwenye matokeo ya darasa la saba

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Matokeo ya Darasa la saba hupangwa kwa Mkoa/wilaya kitu ambacho ni kizuri na hata mtu akitaka kuperuzi shule za Wilayani kwake anaweza kuziona zote kwa urahisi.

Au pengine waweke option ya kufilter, mtu akitaka shule za Mkoa X, au Wilaya Y, shule za wasichana, Wavulana, Shule za ufundi, shule za mrengo wa dini flani, Shule za walemavu nk nknk aweze kupata kwa urahisi.
Wanaweza kwenda mbali na kuweza kufilter ili kujua ufaulu wa somo flani kiwilaya/mkoa nk. Hapa tutajua Wala samaki/Mihogo wanafaulu somo gani zaidi nk nk itaweza kusaidia tafiti nyingine.
Mtu yeyote wakiwemo viongozi, hawatakuwa na haja ya kupiga simu Wizarani kuomba hizo report.

Kwa huu mfumo unaotumika Sasa hivi ukiambiwa utafute shule za Sekondari zilizopo mkoa wa Rukwa kwa mfano au hata Morogoro utaishia kubahatisha pengine shule 4 zile za zamani?

Sioni kwa nini mzazi ahangaike kutafutia mtoto shule pengine Mwanza, wakati kupitia tu matokeo ya mitihani ngazi mbalimbali mtu angeweza kuziona shule zote tena kwa technologia rahisi kabisa. Naamini kuongeza hiyo filter hakuna gharama yoyote kwa sababu IT wa Wizara walio ajiriwa wanaweza fanya tu kama sehemu ya kazi.
 
Ipo Sehemu Ya Kuchagua Herufi Ya Shule Mfano KIBASILA Unakwenda K
 
Ipo Sehemu Ya Kuchagua Herufi Ya Shule Mfano KIBASILA Unakwenda K
Naomba kujua Shule za Sekondari zilizopo Wilaya ya Mbogwe & Wilaya ya Kyerwa; Kuna mtu anatafuta shule nzuri ya mtoto huko. Hebu tumia hayo matokeo, unitajie shule walau tatu za hizo Wilaya?
Ukisikia "AI technologies; ni kuwezesha mifumo isaidie watu na kuwarahisishia maisha
 
Naomba kujua Shule za Sekondari zilizopo Wilaya ya Mbogwe & Wilaya ya Kyerwa
Kuna mtu anatafuta shule nzuri ya mtoto huko
Hebu tumia hayo matokeo, unitajie shule walau tatu za hizo Wilaya?
Ni Lazima Mkuu Ujue Shule Za Huko Majina Yake Halafu Herufi Ya Kwanza Unaitafuta Pale
 
Ni Lazima Mkuu Ujue Shule Za Huko Majina Yake Halafu Herufi Ya Kwanza Unaitafuta Pale
Ndo maana anapendekeza watumie mfumo wa mikoa na wilaya. Itasaidia.

Hii ya sasa inachosa, mpaka ujue unachokitafuta.
 
Back
Top Bottom