Natokwa jasho jingi sana kwapani

MsafiriBM

Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
21
Reaction score
2
Natokwa na jasho jingi sana kwapani kupita kiasi nyakati zote za joto na baridi. nalazimika kubadili mashati hadi mara tatu kwa siku na wakati mwingine navaa koti au sweta kuficha hali hiyo. Kwa yeyote anayefaham tatizo hilo anipe msaada wa mawazo.
 
Nyoa chaka hilo then paka poooda na usivae mashati ya nylon au msweta mazito.
 
Kaogelee baharini kila siku mpaka lirudi kuwa kawaida.
 
Najitahid sana kuzuia hilo chaka mkuu..yaan pako clean.!
 
mkuu pole sana. hilo tatizo lakutokwa na jasho jingi sana linaitwa axillary hyperhidrosis huwapata watu wengi sana mara nyingi linasababishwa
- wasiwasi
- hofu
-unywaji wa kahawa
-uvutaji wa sigara
-magonjwa kama kisukari, TB, Matatizo ya moyo
-vinywaji
-nguo aina ya nylon
-baadhi ya vyakula
kutokana na hali hiyo nerve za sympathetic zinachochea tezi za jasho kutoa jasho jingi

TIBA
-kuepuka visababishi hapo juu
-pima magonjwa kama TB, kisukari ,magonjwa ya moyo, kama utakuwa na dalili zingine
-tumia aluminium chrolide
-botox pia inatumika
-jitaidi kuonana na dactari kwa tiba zaidi na ushauri
 
wakati mwingine ni maumbile tu ya mtu tu ,nimeshaona mtu mmoja mwenye tatizo kama lako akijitahidi kufanya kila awezalo na kujiweka msafi nyakati zote lakini imeshindikana.
 
Umepona kaka wala usiwe na shaka,nenda maduka ya kiasili uliza SHABU,ni elfu moja tu.Ipo kama chumvi.... chota kiasi weka kwenye kikombe tia na maji iwe ndo deodorant yako........UTANAMBIA,Au kama una kishupa cha deodorant kilichoisha weka iyo shabu kiasi na maji then unajipaka kila ukioga....Kwapa liwe jeupe
 
weka vi sponji kwapana viwe vinanyonya jasho ...hiyo ndo suluhu ya tatizo lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…