The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Je, wewe ni mwanamke ambaye umeachwa na huamini tena ktk mapenzi?
Au unaachika kila mahusiano hujui sababu ni nini?
Anyway najua sababu ziko nyingi... inawezekana umekutana na wanaume wasiojielewa lakini leo nataka uwaze kwa upande wako zaidi.
Kuna mambo usipoyajua utaendelea kuwalalamikia wanaume kumbe tatizo ni wewe... sitaki nikuhukumu ila natamani kukusaidia.... be positive in this article.
Utafiti wangu ulijikita kwa wadada 20 walioachika na nimegundua tabia ya hasira za haraka kwa wadada 18 kati ya hao. Nikapima hasira zao ndipo nikaona hata kama na mimi ningekuwa na mmoja kati yao ningemwacha kabla ya kufikia ndoa. Nasema kama mwanaume kwa hiyo mwanamke timamu anaweza kuzingatia hili:
Hasira! Panic! Hasira!
Hakuna mwanaume wa kawaida anapenda kuishi na mwanamke mwenye hasira labda yule aliyetumwa kwako na Yesu kwa mission maalum.
Jaribu fanya utafiti waulize wanaume 10 waulize kama wangependa kuoa mwanamke mwenye hasira then utanipa jibu.
Tafuta wanaume waliooa 10 ambao wake zao wana hasira then waulize kama wanafurahia... utanipa jibu na katika wale wanaofurahia chunguza maisha yao kama hawana magirlfriend wanaopata nao muda wa kuenjoy.
Nazungumza na mwanamke mwenye akili timamu maana hiki ni chakula kigumu.
NINAPOSEMA MWANAMKE MWENYE HASIRA NAMAANISHA MWENYE TABIA ZIFUATAZO:
1. Mwanamke anayekasirika hovyo na lazima akuoneshe kwa vitendo kwamba amekasirika. Atabamiza mlango (wa gari au wa chumba) atamwaga chakula, atarusha kitu, atapiga meza au ukuta.
2. Mwanamke anayenuna hata kwa kosa dogo ( anaweza kuzila kula, kulala chini, kuzima sim, kujifungia ndani, kukataa kupika, )
3. Mwanamke ambaye analazimisha ufanye anachotaka. Wanaume asilimia 98 wanasema wanapandwa kichwani. Mwanamke anapaswa kushawishi na kubembeleza ( atapata kila kitu) ila sio kulazimisha kwa ukali kwa kigezo cha kuwa wewe ni mchumba au mke.
4. Mwanamke ambaye anaongea na mwanaume kwa sauti ya ukali. Mwanaume hata akikosea ukitaka asikuone kero chunga sauti yako mwanamke. Mwambie mumeo ukweli lakini sauti yako ndio itaamua akusikilize au akupuuzie au akupige makofi ( kama hana hekima za kuchukuliana na wapumbavu kama wewe).
Ewe mwanamke. Hasira ni sumu ya kwanza kwa mahusiano yako. Hasira yako inawafukuza wanaume wengi... sisemi uifiche bali uitafutie dawa ipungue ibaki asilimia 5 tu ya kukusaidia kuukasirikia umaskini na ujinga.
HIVI HUJUI AU KIBURI TU? ETI KWELI HUJUI KUWA MUME...
Mume hakunjiwi sura.
Mume hagombezwi
Mume hatukanwi
Mume ni bwana wako sio mtoto wako.
Mume ni kichwa cha familia.
Mume hadharauliwi.
Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu.
Umeona uhusiano wa hasira na upumbavu na kufeli kwa mahusiano katika hayo maandiko ?
Kwa leo niishie hapo. Sio kwamba wanaume wote hawana upumbavu ila kwa leo tuwaache kwanza ili nafsi kadhaa za wanawake zipone . Ni maombi yangu usifeli kwenye mahusiano kwa sababu ya hasira na ukali.
Nimalizie kwa kukupa siri:
WANAUME wote wanachanganyikiwa ukiwaonesha jinsi gani wewe ni mwanamke laini sio jinsi gani unaweza kuwa mbabe kama/kuzidi yeye. Nenda usome vitabu uone jinsi wanaume wababe walinaswa na wanawake wenye kinywa laini.
19/2/2025
FEDRICK Makayula Mahusiano na NDOA