Kumbe bwana hata waafrica tuna nywele ndefu tu kama wazungu
Hii thread Ni maalum kwa watu wenye nywele natural I mean tunaotaka nywele ndefu bila dawa aka relaxer
Hapa tutashare uzoefu Nini Cha kufanya
Mimi kikubwa sana nilichogundua ukiosha nywele zako never ever usizikaushe kwa Moto neither dryer nor blow dryer
First, you have to infuse moisture into your hair. Moisture is simply water. Kuwa na spray bottle yenye maji tu ya kawaida ya kunyunyizia kwenye nywele hata Kama umesuka.
Secondly you have to retain that moisture by locking it in. Lock it in with oil. Penda kutumia mafuta ya mnyonyo-castor oil, mafuta ya nazi or mafuta ya olives.
Thirdly you have to manage your hair from root to end by ensuring that you have a protective hairstyle. By this I mean simple braided hair. (Mabutu tu ya kawaida nywele tatu, tano, nywele za kusokota za kawaida ama za uzi Kama haziumi na hazivutwi Sana) usiziache bila kuzifunga zitakatika.
Another secret to hair growth is the use of rice water. Ukishamaliza kuosha Mchele wako, yake maji ya mwisho kabisa yatumie kunyunyizia kwenye nywele zako japo Mara Moja kwa wiki. Baki nayo kichwani na ubae shower cap kwa muda wa lisaa Moja. Then suuza vizuri na uendelee na step zingine.
Mzungu ndio reference au sio..duh..kwel africa tuna safar ndef.....ndomana hamwach kuweka kucha kope.nywele.ngozi na makeup bandia kila kukicha..yaan inaonyesha bado ndugu zetu nyie hamjajikubal kabisaaa.duh..hali ni tete...ndo mana mnajichubua..sorry lakin nime come out strong kwenye uz wako
Steaming walau mara mbili kwa mwezi..pendelea zaidi vitu vya asili mfano parachichi, asali, ndizi, tui la nazi, maji ya mchele, maji ya vitunguu maji, mayai, maji ya ya tangawizi ni mazuri sana kwa wenye mba.
Ukiosha waweza kutumia bamia kama leave in conditioner, kisha ukapaka mafuta yako ukasuka.
Kama una uwezo na unapenda nywele zako zitunze kwa kutumia vitu asilia au genuine products kama utalazimika kununua....napendelea kutumia shampoo kutoka dove na hot oil treatment za vatika hii naitumiaga kama conditioner so kama una kipilipili bidhaa hii ni nzuri sana kuchania nywele wakati wa kusuuza na kuzifanya ziwe soft muda wote.
Tip nyingine ukiosha nywele usikaushe kwa taulo Ina tabia and ya kushika ncha za nywele na kuzifanya zikatike ovyo, tumia vitambaa vyenye nyuso laini mfano Mimi nimetenga mitandio ya dira maalum kwa kazi hiyo.
Usiache nywele bila kupaka mafuta baada ya kua umeziosha kwa shampoo na huna conditioner/mask.......unaweza kuziacha na unyevunyevu wake Kisha paka mafuta mengi sana, funga kitambaa kama ni usiku uje uzichane asubuhi, zitakua soft na hazitakatika hata kidogo. Au baada ya kuosha especially mida ya mchana unaweza koroga parachichi ukapakaa na kuliacha likaukie humo baadae ukichana nywele mabaki yake yataanguka tuu no need kuosha tena.
Miongoni mwa home made treatment's combos unazoweza kujaribu na kujua ipi inakufaa zaidi.
Tui zito la nazi + parachichi
Home made mayonnaise,.....yangu nachanganyaga kiini cha yai la kienyeji olive oil, kitunguu thomu, ndimu na rai....hii kwangu ni the best kwa usumbufu wa aina yoyote.