Natural justice ni haki ya kila mtuhumiwa au inategemea na aina ya mtuhumiwa?

Natural justice ni haki ya kila mtuhumiwa au inategemea na aina ya mtuhumiwa?

aduwilly

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
1,180
Reaction score
307
Naomba nianze nukuu mbili za waziri mkuu mstaafu EL alizotoa bungeni wakati akichangia repoti ya iliyokuwa kamati teule chini ya uenyekiti wa mtunzi wa kitabu cha "Pepo ya Mabwege" ndg. H. Mwakyembe.

"Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice". Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja"

Nukuu ya pili ni hii

"Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni?"

Mwenyekiti wa kamati teule wakati anahitimisha hoja yake alisema kuwa hawakumuhoji kwa vile walijua kutokana na wadhifa wake anaweza kuharibu ushahidi.

Swali ni je natural justice ni haki ya mtuhumiwa yeyote au inategemea na status yake ili hali no one is above the law?
 
Wakati mwingine0hawa wazee wakizeeka akili huwa znarudi utotoni mpaka mwenyewe na shindwa kufahamu kaka.
 
Hapo hawakumtendea haki. Huwezi hukumu mtu wakati hujamsikiliza.
 
natura justice na katiba ya jamhuri ya muungano 1977 ikataza kwa mtu yoyote kuadhibiwa bila ya kupewa nafasi ya kusikilizwa
 
Back
Top Bottom