[emoji991]Pichani ni mikoko yenye afya katika eneo linalosimamiwa Bagamoyo, na isiyo na afya katika kijiji cha Mdimni, Mkuranga nchini #Tanzania. Mikoko hii imeathiriwa na shughuli za wanadamu na mabadiliko ya tabianchi, na kusogea kwa maji ya bahari.
Leo Jumanne ni Siku ya Mikoko Duniani.
Je, unajua kuwa hekta moja ya mikoko ina uwezo wa kuhifadhi tani 3,754 za kaboni, sawa na kaboni inayotoka kwenye magari 2,650 kwa mwaka?