Nauadabisha mwili na tamaa zake, siyataki mapenz yangu tena

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Uzi huu utaonekana una udini kidogo, lakini kikubwa ni kuwa nataka kuonesha jinsi gani wakati mwingine tunachokitaka sisi binadamu katika maisha hakina umuhimu sana na mwisho wake ni mbaya.

Mwili wangu unataman kula vyakula vingi vitamu bila kujali napata nin.
Mwili wangu unataman ninywe pombe, kulewa kila wakati.
Mwili wangu unataman nifanye kazi masaa machache na kustarehe sana.
Mwili wangu unataman kuchelewa kuamka.
Natamani kuheshimiwa na kila mtu na kupewa sifa.
Mwili wangu unataman niwe na mpenz zaidi ya mmoja, nibadili mpenzi kila siku.
Natamani kuowa/ kuolewa kwa ndoa ya kifahali.
Mwili wangu unataman kuvaa mavazi mazuri na yakuvutia
Mwili wangu unataman kutenda kile ambacho moyo wangu unataka wakati wote.
Mwili wangu unataman nifurahi na kucheka na ndugu na rafiki zangu.
Natamani niwe na watoto wengi na mwenza pia.
Natamani kutembea kona mbali mbali za dunia na kuona vitu vizur mbalimbali.
Natamani kupata mali kwa njia rahisi hadi naamua kuiba.
Mwili wangu unataman kupewa sifa na wandamu kuwa ni mimi nimewapa msaada.
Nataman kuonekana mtu mwema na mwenye upendo na akili nyingi za kimaisha.

LAKINI HAYA YOTE SI KITU KWAKO MUNGU.
najua wew huandiki makosa yangu bali wataka nikuabudu tu na kufanya yaliyo mapenz yako.

Sasa naudabisha mwili na tamaa zake.
Nitafanya kazi masaa 12 kila siku huku nikitafakar yaliyo mapenz yako.
Nitajifunza neno lako ewe Mungu kila wakati
Nitasikiliza sauti yako kila wakati
Nitafanya mazoezi ya viungo kila siku.
Natajituma sana na sita kuwa mtu wa kutuma wengine.
Nitapendezwa na wanaokujua wew Mungu na kulieneza jina lako.
Sitaki tena kufanya yalio mapenz yangu, nitafanya kazi yako sawa sawa na neno lako.
Sitaki tena kufalijiwa na wanadamu bali wew pekee.

Nahakika magonjwa na maradhi ya kila aina hayawezi nipata kunikwamisha kufanya yalio mapenz yako.
Mithali 30:7-9
[7]Mambo haya mawili nimekuomba;
Usininyime [matatu] kabla sijafa.
[8]Uniondolee ubatili na uongo;
Usinipe umaskini wala utajiri;
Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
[9]Nisije nikashiba nikakukana,
Nikasema, BWANA ni nani?
Wala nisiwe maskini sana nikaiba,
Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.

YALIO MAPENZ YANGU SITAKI TENA.

Tuungane pamoja kuuadabisha mwili na tamaa zake.
 

Utaepuka kulia
 
hizo zote ulizoandika ni pumba maana bado utarudi huko huko, labla ujiue ndo itakuwa jambo la msingi.
 
hizo zote ulizoandika ni pumba maana bado utarudi huko huko, labla ujiue ndo itakuwa jambo la msingi.
Hujui raha ya kusemeza na roho mtakatifu wew.
Faida yake haifananishwi na chochote hapa duniani.

Sorry kama huto nielewa.
 
Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Yasio wezekana kwa mwandamu, kwa Mungu yanawezekana.
Anaweza kukubadilisha.
Kweli kabisa.
Kusali, kufunga na kuomba.
Tena uwe mtu wa maombi ya mzigo.

Mungu hashindwi kurekebisha tabia au tamaa za mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…