Nauli kupanda mzigo juu ya mzigo kwa masikini sisi

Nauli kupanda mzigo juu ya mzigo kwa masikini sisi

Joined
Jan 17, 2013
Posts
37
Reaction score
4
Habari gani wanajamii natumai ni wazima na maisha yanaendelea ingawa hayana uhakika sana kama hata kesho itakua hivi au tofauti na hivi.ndugu zangu leo ninasukumwa kuandika haya kwa sababu ya ONGEZEKO LA KINYAMA KWENYE NAULI nashawishika kuliita la kinyama kutokana tu na hali halisi ya maisha ya huyu mtanzania wa kawaida kama mimi ninaye uziwa kilo moja ya mchele kwa sh 2000-2400 sukari kilo 2000 unga nao bei haitambuliki.lakini hiyo haitoshi sasa naongezewa mzigo zaidi kwenye nauli jamani kwa hali ya kawaida kabisa embu tuangalie mtu anaishi gongolamboto anafanya kazi mwenge kwa nauli hizi analazimika kulipa zaidi ya sh 36000 kwa nauli hii ya sh 600 anayolipa sasa mtu huyu anawatoto watatu wnaosoma shule ya kutwa hapa mjini kila moja analizimika kumpa tsh12000 kwa mwezi kwa ajili tu ya nauli na gharma zingine sasa chukua huyu mtu anapata mshahara kiasi gani?kumbuka yeye ni mtz tu wakawaida jibu ni hatari kulijua mana litatupa kazi nyingine tena njoo kwa wenzangu wamikoani inatisha kwa kweli maisha magumu yalikua sasa nimagumu sana na yanazidi kuongezwa ugumu zaidi

LAWAMA;;
1:serikali
2:sumatra
3:taboa
Serikali imeshindwa kulinda raia wake imeshindwa kusimamia haki na na hitambuhi wajibu wake!!!!

Sumatra haina mchango na haitambui uwepo wake kwa watanzania na uwepo wke kisheria

Inajali faida na sio uzalando kwa taifa hili

Just nime mention maana naamini majibu haya mnayo na maelezo pia

MWISHO;

Swali hili ni rahisi sana na ndio point kwa wote

Mafuta hayaja panda kwanini?ongezeko la nauli????
 
Back
Top Bottom