KERO Nauli ya Banana – Kivule (Fremu 10) ni mateso kwa Wananchi. Gharama zipo juu, Mamlaka ziingilie

KERO Nauli ya Banana – Kivule (Fremu 10) ni mateso kwa Wananchi. Gharama zipo juu, Mamlaka ziingilie

  • Thread starter Thread starter Anonymous (1fdd)
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kabla ya nauli kupandishwa mwishoni mwa mwaka jana nauli ya daladala kutoka Kivule fremu 10 hadi Banana ilikuwa 500/=. Baada ya serikali kupandisha nauli toka 500/= kwenda 600/= daladala za huku zimepandisha nauli kutoka 500 hadi 1,000/=

Tunaomba LATRA na mamlaka husika zitusaidie sisi wananchi tunatumia gharama kubwa kwenye nauli
 
Poleni sana, huenda barabara mbovu sana hivyo kuharibu magari mara kwa mara.
 
Mara nyingi mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa. Viongozi wengi na wenye mamlakani kama huwa hawafahamu ugumu wa maisha tunaopitia sisi watu wa chini maisha ni magumu mno sijui kama viongozi wetu hasa wabunge wanalitambua hilo.
 
Mbunge wenu yuko bize kumfurahisha mama Kwa uhuni uliofanywa na serikali ya CCM, Jimbo la Ukonga miundo mbinu ya barabara ni majanga
 
Malalamiko yangu ni sisi Wakazi wa Kivule hasa Kivule Fremu Kumi, kuna muda hasa kipindi cha mvua kutoka Banana hadi Fremu 10 mtu mmoja unajikuta umetumia nauli kati ya Shilingi 2,000 hadi 5,000 kutokana na usafiri kiwa shida.

Kinachouma zaidi ni kuwa kipindi hiki mvua hakuna na barabara imekwanguliwa nauli inacheza kati ya Shilingi 1,000 hadi 3,000 kwa kutegemea na chombo cha usafiri.

Naomba Serikali kupitia TAMISEMI, LATRA, TARURA na hata HALMASHAURI ya JIJI iingilie kati ili unafuu urudi.

Maisha ni magumu, kuendelea kuwekewa gharama kubwa ya nauli kama hivyo ni kutuumiza Wananchi hasa sisi wenye kipato cha chini.
 
Back
Top Bottom