Malalamiko yangu ni sisi Wakazi wa Kivule hasa Kivule Fremu Kumi, kuna muda hasa kipindi cha mvua kutoka Banana hadi Fremu 10 mtu mmoja unajikuta umetumia nauli kati ya Shilingi 2,000 hadi 5,000 kutokana na usafiri kiwa shida.
Kinachouma zaidi ni kuwa kipindi hiki mvua hakuna na barabara imekwanguliwa nauli inacheza kati ya Shilingi 1,000 hadi 3,000 kwa kutegemea na chombo cha usafiri.
Naomba Serikali kupitia TAMISEMI, LATRA, TARURA na hata HALMASHAURI ya JIJI iingilie kati ili unafuu urudi.
Maisha ni magumu, kuendelea kuwekewa gharama kubwa ya nauli kama hivyo ni kutuumiza Wananchi hasa sisi wenye kipato cha chini.