Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Ameandika Zitto Kabwe kupitia X:
Nimeona mjadala mkali kuhusu Tanzania kununua Umeme kutoka Ethiopia. Bahati mbaya mjadala umejikita kwenye umbali (distances). Ni muhimu kuelewa biashara katika sekta ndogo ya Umeme.[Watu wanaonekana kuuliza kwamba, kama umeme unaleta hasara kutokana na kusafirishwa umbali mrefu, huo umeme kutoka Ethiopia kuja Tanzania kupitia Kenya hausababishi harsara kwa sababu ya upotevu?]
Kwenye biashara ya umeme (cross border power trade) ukinunua umeme kutoka nchi A umeme huo huusafirishi mpaka nchi B.
Umeme unawekwa pamoja (power pool) kisha nchi zina 'trade' kati ya 'surplus countries' na 'deficit countries'.
Mfano Tanzania ikinunua 100MW kutoka Ethiopia, Ethiopia inaweka umeme huo kwenye gridi ya Kenya na Kenya inaipa Tanzania 100MW zote katika Kituo cha nguvu ya umeme kilichopo mpakani.
Kwa maana hiyo Tanzania inapokea 100MW Namanga mkoa wa Arusha. Tanzania haichukui 100MW nchini ethiopia kwenye chanzo na kuusafirisha mzigo kama gunia la viazi kwenye lori, la hasha.
Tanzania inachukua mzigo wake mpakani. Ni kama unapotuma pesa kwa M-Pesa. Pesa zile hazitembei kutoka wakala mmoja kwenda mwengine. Unachukua kutoka float ya wakala anayekupa. Umeme ni hivyo hivyo.
Tanzania hiyo hiyo ikizalisha umeme Rufiji inausafirisha mpaka Arusha kwa sababu ni gridi moja.
Transmission loss ya kutoka Rufiji mpaka Arusha yaweza kufikia 15-20% ilhali hakuna significant transmission loss kutoka Namanga kwa sababu umeme unaingia kwenye matumizi moja kwa moja kwa kupozwa kwenye power stations kutoka 400kv mpaka 66kv mpaka 33kv mpaka 11kv za majumbani. Hoja ya msingi inayopaswa kujibiwa na Serikali @MsigwaGerson ni haya:
- Je, Umeme wa ziada tunaozalisha tunaupeleka wapi?
- Kama ambavyo Ethiopia inauza umeme wake wa ziada, Tanzania inapeleka wapi ziada?
- Je tukinunua umeme ethiopia na sisi kuuza kwa nchi jirani tutakuwa 'net exporters' au 'net importers' wa umeme?