Nauliza wako wapi watu hawa?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001


Watu wa Juma Nature
Sonia,Mzee Mwalubadu,Mzee wa Busara, Mtoto Idi kazua balaaa!!.

Mtoto wa Geti Kali wa Inspector Haroun

Sokomoko, Pimbi,Mwindaji Komredi Kipepe, Dokta Love, Ndumilakuwili, Lodilofa, Striker Matata Mapung'o (aka Meddie Kagere) wa timu ya Bus Stars. Zena na Betina, Mwinyi Mpeku na wale madogo wachafuzi wa lugha. Hawa walitajwa sana na jarida la Sani

Sadiki na Chitemo, Mtoto Mzuri Mussa na Neema,Mfalme aliyekuwa na masikio kama Punda, Manahodha waliozamisha meli kwa kuzidiwa na utamu wa muwa.

Msanii Babu Ayubu, Mike Tee Mnyalu, Stars Thomas, Kali P nk
Ongeza na wengine. Kimsingi hawa nilikuwa nawasikia tu nikiwa nasoma shule ya msingi kijijini kwetu.

Nahitaji kujua wamepotelea wapi kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…