Naulizia chimbo la "smart watch" halisi

Naulizia chimbo la "smart watch" halisi

shamzugi

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2021
Posts
535
Reaction score
1,115
Habari wakuu?

Niende moja kwa moja kwenye mada, nilikua nahitaji smart watch halisi, isiwe fake, lakini pia iwe na mwonekano mzuri, namaanisha isiwe ndogo sana. Mkinisaidia Aina ikiambana na picha itakua mzuka Sana.

Karibuni


Screenshot_20230619-004111.png
 
Huawei GT2, ninaitumia inakaa na chaji wiki mbili.

Inamuonekano mzuri
Unaweza kubadilisha mikanda
Haiingizi maji
Haichakai haraka

Unaweza ku google kuifahamu zaidi ila ni saa moja nzuri sana

71xNCOg7LWL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg
 
Ahsante Sana mkuu, naweza kuipata wapi na Bei yake tafadhali
Kuna duka lipo dar Instagram wanajiita phonepointdar niliona wamepost wanayo.

Ila mimi niliagiza Aliexpress iligharimu $136 ilikuwa December 2021. Naimani kwa sasa gharama itakuwa imepungua.

Niliagiza huko Kwa sababu wakati nahitaji maduka mengi hawakuwa nayo. Ila badae nilibaini huko gharama ilikuwa nafuu kuliko kununua hapa nyumbani.
 
Naomba nifunge mjadala kwa kumshauri kama anakipato cha chini kwa sasa haylou solar rts 3 haina mpinzani .Ila aseme anahitaji kwa matumizi gani ? Kuna second hand za sasmung mfano watch 3 pia hadi usd 50 unazipata aliexpress
 
Back
Top Bottom