Naulizia gharama za kuunga umeme wa TANESCO

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
1,736
Reaction score
408
Wakuu naomba mnijuze gharama za kuvuta umeme wa TANESCO kwa sasa ziko vipi kwa single phase na double phase maana ninafikiria kuweka umeme kwenye kibanda changu, Nguzo ya karibu ni ya single phase na ipo umbali wa kama mita 50 hivi toka kwenye hako kabanda kangu.
 
1.Maombi ya mwanzo 6000/
2.Mchoro wa nyumba na kusaini fomu single ph 50000/
3.Survey bure
4.Service line bila nguzo 45500/
Hizo ndizo hatua muhimu na gharama halisi lakini kama ni mt50 bila sha itahitajika nguzo!
Tumia mkandarasi aliyesajiriwa kuepuka vishoka kuchora na kuisaini fomu ya maombi!
 
Uvute umeme upi wa tanesko?? We huoni giza kila siku?? Hiyo gharama unayotaka kutoa kuvutiwa umewe hewa wa tanesko, tafadhali nenda kanunue soler funga na utafurahia kuwa mwangani siku zote
 
Uvute umeme upi wa tanesko?? We huoni giza kila siku??wenzio tunatafuta pa kutokea we unatafuta pa kuingilia,Hiyo gharama unayotaka kutoa kuvutiwa umewe hewa wa tanesko, tafadhali nenda kanunue soler funga na utafurahia kuwa mwangani siku zote
 
Yericko umekosea kidogo, Minimum ie withn 30m ni 455,105/, application card ni 5,900. Kama ni 50m lazma one pole, gharama ni 1,352,000/, kama ni 120m bas ni 2poles gharama ni 2,002,000 bei zote hz Vat iclusive. Siku hz pia kuna Akiba bank wanatoa mkopo wa kuunganisha umeme kwa watu wasio vizur kimfuko.
 
Hizo gharama ndio halisi ila nenda Tanesco uone kazi.....Ukitaka kutoa hizo pesa na si zaidi utaambiwa uje mwakani mwezi wa 2 kisa na sababu ndio kwanza wamepanda miti ya nguzo iringa subiri ikue na ivunwe ndio ije kuwekwa eneo unalotaka.....
 
hahahaa! Thats fantastic!
 
Hiyo nguzo kwa bei ya 1,352,000/= ni wizi mtupu. Bora tuagize nguzo za chuma toka China haitazidi 300,000/=.
Ukitaka kujua kama tunaibiwa ni kwamba nguzo hiyo ukilipia kwa kiasi hicho bado inakuwa mali ya Ta4sco!
 
zinapatikana wapi hizo nguzo za chuma? tanesko wanazikubali? msaada please!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…