Naumia, nami ni binadamu

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,476
Reaction score
11,659
Kwa marafiki na jamaa wa JF.

Mwaka 2018 nilipata tatizo la ghafla na kuugua,na pia sikua na uwezo ama kujiaandaa kukabiliana na hill tatizo.kwani nlitoka kwenye kipindi kigumu cha kumuuguza ndugu yangu na sikua na kipato,hali ilivozidi kuwa mbaya ikanilazimu kuomba msaada kwa baadhi ya marafiki wa jf,kuna watu walijitokeza na kunisaidia kupata 300K ya bima ya Afya nkaleta na mrejesho.

Lakini tatizo liko hapa;

Kuna baadhi ya member mnaniweka kwenye masikitko na huzuni,its like Mimi ndo wa kwanza kupata matatizo na kuomba msaada JF? Imekua too much kwa sasa,lisitokee jambo mtu kaibuka na kuongeea msaada nliopata,kuna wengine mnafikia hata ya kunidhalilisha kwa makosa yasiyojulikana,makosa ambayo siyajui na hapana ukweli kabisa.

Kuna mda mwingine nakubali nakosea,nakubali na naomba mkumbuke Mimi ni binadamu kama wengine sio malaika.
Lakini kinachoshangaza na kuumiza mtu anakuja na kuingiza habari za msaada kwenye hayo masuala..its inhumane.
I appreciate what you did to me,ni kitu kikubwa ambacho kilinisaidia mno, lakini the way mnavolikuza na kuliongelea ni kama nlipewa mkopo na si msaada wa kibinadamu.

Whenever you get a chance u use it to insult me, why? Mimi ndo wa kwanza kuomba msaada humu JF? Kama kwenye matatizo wote wangetreatiwa hivi ni yupi angekua na amani mbele za watu?

Guys, nilipoteza wazazi wote wawili nikiwa mdogo sana. Nikachukuliwa na familia ya mtu, nikakua kwao, lakini kila nikikosewa au kufanyiwa ubaya kama binadamu nikiongea kuonyesha nilivokereka maneno nitayorudishiwa ni "huna baba wala mama, tumekulea hadi umekua n.k.

Ninapopokea kauli kama hizi natamani nifanye malipo,angalau kupunguza maneno, lakini malipo ya wema na utu ntayalipaje, kama ni chakula nitawalisha nikifanikiwa.

Na kwenu pia, nashukuru sana kwa mda wenu, kujitoa kwenu na upendo wenu mlioonyesha na Mwenyezi Mungu atawalupa kwa hili. Lakini kwa upande wa pesa angalau ntawalipa.nko imara kwa sasa hapo sio kikamilifu lakini nna nguvu ya kufanya mengi ukilinganisha na mda uliopita.

Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu nirudishe kidogo kidogo angalau maneno yapungue maana najiona nina deni kwa jinsi hali ilivo.

Watu walionifanikisha msaada wapo 13, kipindi napokea msaada niliwanote kwenye diary, na wote nawajua I'd zao na amount ya kila mmoja na nitajitahidi taratibu kurudisha angalau nipate nafuu.

Nawapemda wote

Aggy
 
Pole sana aggyjay

Siku zote dawa ya mjinga ni kumnyamazia na huwezi kuzuia mtu kuongea/kuandika anachotaka...sometimes ni suala la kuignore unachokisoma

Unadhani ukiwarudishia hizo pesa ndio watakosa cha kukuattack?kimsingi ningekuwa mimi nisingerudisha hata cent,hukushikia mtu bunduki akusaidie na haitasaidia chochote kwao kuendelea kuongea

Ni ngumu sana kumplease binadamu na huwezi kupendwa na kila mtu
 
Asante joanah..but kuna mda mwingine naelemewa na masimango ya watu.najiona nna mzigo

Jifunze tu kupotezea,ndio binadamu tulivyo....

Wapo watu furaha yao ni kuona mtu fulani anaumia,na kwa huu uzi wako watu wa namna hiyo utakuwa umewapa ushindi wa walichokuwa wanataka

Usijione una mzigo kwa watu ambao sio muhimu katika maisha yako
 
Pole sana.

Tatizo la kwetu binadamu tunapenda baada ya kusaidia tunyenyekewe. Yaani nikishakusaidia nihakikishe unakuwa chini yangu, kila kitu ninachosema ujibu yes, ikitokea ukinipinga ndiyo shida inaanzia hapo.

Pole sana, Mungu akutie nguvu ni kweli inauma na yanaumiza sana.

Be strong lady...! You were given this life because you are strong enough to live it.
 
Asante B..umeyaelewa yote nloyasema
Hujakosea hata moja.
Nimeyashinda mengi lakini kuna mda naelemewa kama binadamau
 
Jifunze tu kupotezea,ndio binadamu tulivyo....

Wapo watu furaha yao ni kuona mtu fulani anaumia,na kwa huu uzi wako watu wa namna hiyo utakuwa umewapa ushindi wa walichokuwa wanataka

Usijione una mzigo kwa watu ambao sio muhimu katika maisha yako
Asante.nimekuelewa
 
Pole sana mkuu.
Kwanza ingekuwa mimi ndio wewe nisinge funguwa uzi wa sonona, na zaidi ningewakaushia kana kwamba siwajui, nakwa roho mbaya nisinge badili hata ID, na pesa zao nisinge warudishia.
Pole kwa changamoto unazo pitia, nakukumbusha tu kwamba hii ndio Jf.
 
Acha kujipa mawazo hasi, na pia jitahidi uwe jasiri ktk kushukuru kwa kila jambo upatwalo nalo ktk maisha 7bu hujui Mungu anakuandaa uje kuwa na hekima kiasi gani kupitia changamoto unazokumbana nazo sasa hivi utapofanikiwa kesho ili usaidie Watu wengine kama ilivyokutokea leo hii.
 
Sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…