Naunga mkono kwa asilimia mia Serikali kutoagiza Chanjo ya Corona kutoka nje

Verily Verily

Senior Member
Joined
Jan 4, 2007
Posts
192
Reaction score
148
Naiunga Mkono Serikali kwa ASILIMIA MIA isiruhusu wala kuagiza CHANJO ya Corona. Hii ni kutokana na taarifa zinazozunguka kuhusu uwezekano wa chanjo kutokuagizwa kuleta hapa nchini.

Hii ni kutokana na mwenendo mzima wa hali ya Ugonjwa Duniani ambayo inaweza kutuoatia taswira ya chanjo yake. Mataifa yaliyoingia mkenge wa kufuata miongozo toka huko yamepata madhara makubwa sana ya Ugonjwa huo.

Itakuwa ni Lisa kubwa sisi kama Taifa kuepuka madhara kwa kukataa vipimo na miongozo yao halafu tukapokea hizo chanjo. Nachelea kuweka tunaweza kulipa gharama kubwa sana!

Kuna taarifa za kutosha kuonesha kuwa ugonjwa wenyewe ulitengenezwa katika maaabara hizohizo ambayo chanjo nazo zinatengenezwa.

Ugonjwa wa Corona pamoja na mambo mengine unalenga kwenye global dominance, imperialism, guess za kibiashara na kuweza kufikia maliasili za mataifa yote. Yapo malengo mengine pia. Ni guess muhimu kujiepusha kuingizwa katika mipango hio hatari.

Ikumbukwe pia kuwa sio Corona tu Bali chanjo nyingi (sio zote) zinaletwa kwa malengo maovu dhidi ya afya zetu.

Mwisho watu binafsi watakaoitaji kuvanjwa iwapo tu ni lazima katika kusafiri basi wazipate kwenye vituo maalumu na wawekwe karantini warejeapo nchini mpaka hapo wataalumu watakaporidhika kama hawezi na kuwaambukiza wengine.
 
Pole sana,nahisi una usomi wa namna fulani lakini bahati mbaya huna ufahamu wowote kuhusiana na chanjo zinavyotengenezwa ,zinavyojaribiwa na zinavyotumiwa.Umechanganya siasa na science ni hili ni janga.

Leo hatuuoni ugonjwa wa surua si kwa sababu ya maombi ya siku saba wala kuvukiza bali ni kwa sababu ya chanjo ya surua.

Suala la Corona lina mkanganyiko hasa hapa kwetu Tanzania lakini kwa kuwa tumelifanya ni suala la Usalama wa Taifa basi tukae tuache maji yachukue mkondo wake ila nimesikia mahali ya kuwa pesa za mwenge zitumike kwenye makabilano na corona (nahisi kuna uwezekanao wa second wave).

La pili,epuka sana kutumia neno mabeberu kwani si serikali wala wananchama wa chama kikuu wameweza kutuonyesha mabeberu ni akina nani.
 
Kwa wewe unayekaa Kondoa hata bila chanjo mambo yataenda.

Ila kwa wale wanaofanya shughuli za kimataifa kama biashara za kimataifa hawataweza kusafiri bila card ya chanjo ya Corona.

Itabidi Tanzania ifunge mipaka iwe kama kisiwa.
 
Suala la ugonjwa wa CORONA ulitengenezwa halipo. Ugonjwa wa CORONA ni GOD creation kama magonjwa me3ngine yatokanayo na VIRUS kama surua. ebola, HIV n.k na magonjwa yote yatokanayo na virus basi hudhibitiwa kwa chanjo full stop.

Kwa nini CORONA haikuchukua kasi Tanzania kuna sababu za kisayansi na wala siyo sijui Yesu ametukinga. Hili nitalieleza katika uzi mwingine.

Futa kabisa mawazo ati CORONA ni ugonjwa wa kutengenezwa,m Haitawahi tokea binadamu atengeneze kitu chenye chembe za uhai zinazoongezeka never, never onearth. Mfano watu wanaweza kutengeneza robot 100, lakini hizo robot haziwezi kuzaliana.
 
[emoji22][emoji22][emoji17][emoji36][emoji21][emoji22][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Umewahi kusafiri kwenda ughaibuni mleta mada? !

Kama bado usije kushangaa siku unataka kuingia nchi fulani unaombwa cheti kinachothibitishwa ulichanjwa!
 
Suala la ugonjwa wa CORONA ulitengenezwa halipo. Ugonjwa wa CORONA ni GOD creation kama magonjwa me3ngine yatokanayo na VIRUS kama surua. ebola, HIV n.k na magonjwa yote yatokanayo na virus basi hudhibitiwa kwa chanjo full stop.
Kwa nini CORONA haikuchukua kasi Tanzania kuna sababu za kisayansi na wala siyo sijui Yesu ametukinga. Hili nitalieleza katika uzi mwingine.

Futa kabisa mawazo ati CORONA ni ugonjwa wa kutengenezwa,m Haitawahi tokea binadamu atengeneze kitu chenye chembe za uhai zinazoongezeka never, never onearth. Mfano watu wanaweza kutengeneza robot 100, lakini hizo robot haziwezi kuzaliana.
Mkuu wewe umewezaje kujua hali ya corona hapa Tanzania hali ya kuwa hatupimi corona?
 
Wazungu huwa wanachanja hadi mafua na kuna siku niliingia kwenye pharmacy moja huko majuu wakaniuliza kama nahitaji kuchanja mafua, lakini sijawahi kuzisikia huku kwetu. Inawezekana hata korona ikabaki kuwa ugonjwa wenye madhara zaidi kwa wazungu kuliko ngozi nyeusi na hivyo kukawa hakuna umuhimu mkubwa wa kuchanja huku kwetu..
 
Naiunga Mkono Serikali kwa ASILIMIA MIA isiruhusu wala kuagiza CHANJO ya Corona. Hii ni kutokana na taarifa zinazozunguka kuhusu uwezekano wa chanjo kutokuagizwa kuleta hapa nchini.

Hii ni kutokana na mwenendo mzima wa hali ya Ugonjwa Duniani ambayo inaweza kutuoatia taswira ya chanjo yake. Mataifa yaliyoingia mkenge wa kufuata miongozo toka huko yamepata madhara makubwa sana ya Ugonjwa huo.

Itakuwa ni Lisa kubwa sisi kama Taifa kuepuka madhara kwa kukataa vipimo na miongozo yao halafu tukapokea hizo chanjo. Nachelea kuweka tunaweza kulipa gharama kubwa sana!

Kuna taarifa za kutosha kuonesha kuwa ugonjwa wenyewe ulitengenezwa katika maaabara hizohizo ambayo chanjo nazo zinatengenezwa.

Ugonjwa wa Corona pamoja na mambo mengine unalenga kwenye global dominance, imperialism, guess za kibiashara na kuweza kufikia maliasili za mataifa yote. Yapo malengo mengine pia. Ni guess muhimu kujiepusha kuingizwa katika mipango hio hatari.

Ikumbukwe pia kuwa sio Corona tu Bali chanjo nyingi (sio zote) zinaletwa kwa malengo maovu dhidi ya afya zetu.

Mwisho watu binafsi watakaoitaji kuvanjwa iwapo tu ni lazima katika kusafiri basi wazipate kwenye vituo maalumu na wawekwe karantini warejeapo nchini mpaka hapo wataalumu watakaporidhika kama hawezi na kuwaambukiza wengine.
Is this reality or?
Cooking for the sake of cheo,madaraka?
 
Nadhani watanzania wengi hawafahamu suala zima la covid-19. Mie nadhani muongozo unaotolewa au uliotolewa na WHO haukuwa na lengo la kuleta janga. Sioni sababu ya organization hii kuanza kasumba za kisiasa.

Kiufupi tulipofikishwa sasa ni gizani, haijulikani kama tatizo lipo la covid-19 au halipo. Kitu kimoja ambacho naweza kusema kwa uhakika, covid-19 inasumbua zaidi kwenye hali ya hewa ya baridi. Hii tumeona wakati wa summer tatizo lilikuwapo lakini lilikuwa ni dogo na nchi nyingi ziliondosha lock-down au kupunguza masharti. Ilipokija baridi zimerudia pale pale kwenye hard-lock down.

Huu ni ushahidi tosha kuwa TZ kwa hali ya hewa yake inawezekana tatizo likwa ni dogo kuliko nchi za baridi au magharibi. Mie si daktari pengine wenye elimu zaidi watatuekea sawa.
 
Back
Top Bottom