JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Huku mtaani kwetu suala la ulinzi shirikishi ni kama limekuwa linachukuliwa poapoa hivi, kuna wengine wao wanajiona wapo salama labda kutokana na mazingira yao ya nyumba zao kuwa na geti au kuwa na walinzi.
Wengine wanaona ni ubahiri kutoa fedha kwa vijana au watu wanaofanya kazi ya kulinda mtaani usiku, ni wazi kuwa inawezekana haipo kisheria lakini hiyo haimaanishi kuwa siyo kazi nyepesi.
Mara kadhaa nimeona viongozi wetu wa Serikali za mtaa wanaanzisha kampeni hiyo ya kulinda lakini wale wanaojiona wajanja wanapotezea kutoa ushirikiano, hii siyo sawa.
Nimeona Serikali ya mtaa flani hivi Kijitonyama wanasema kuwa wale ambao hawatalipa fedha kama motisha kwa vijana wanaolinda watawapeleka Mahakamani, mimi binafsi naunga mkono hoja hiyo.
Haohao wanaogoma siku wakivamiwa au wakiibiwa ndio wanakuwa wa kwanza kutoa lawama kwa Polisi na Serikali, hivi wanadhani Serikali na Polisi zitakuwa na kazi ya kumlinda kila mtu muda wote?
Mambo mengine tujiongeze tu wenyewe tu tutumie akili za kuzaliwa, siyo kila kitu iwe sheria.
Pia soma: Kijitonyama: Wananchi wanaokataa kulipia ulinzi shirikishi kupelekwa Mahakamani