Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Kuna msuguano wa kufurahisha kidogo wa Tff na Yanga. Imefika mahali sasa ni kama anatafutwa nani zaidi katika taasisi hizi mbili.
Kwangu wa kulaumiwa kwa kutufikisha hapa ni Tff. Mtoto umleavyo ndivyo akuavvyo. Kama mliwazoesha kupindisha sheria Kila walipohitaji kufanya hivyo kwa nini Leo mnawagomea?
Mliwaaminisha wao ndio Kila kitu na Kamwe wao lao haliwezi kupingwa. Sasa kwa nini Leo mnaonyesha sura tofauti?
Bifu hili lilianzia pale Mkwakwani na kwa kuwa walijua wanawaweza na wanawamudu ndio maana yalitokea yale yaliyotokea. Na tuwe wakweli sakata lile kama sio mwandishi mmoja kuliibua na kuliweka hadharani lingefukiwa na lingefumbiwa macho. Kama mlivyowazoesha wakafanya kama kawaida kuwahi kuchomoa line ila wakawa wamechelewa.
Ni Tff hii hii ambayo ililalamikiwa sana msimu uliopita kwamba imepanga kuwapa yanga ubingwa na ikafika mahali kiongozi wa Simba akatamka maneno makali kiasi Cha kupewa adhabu ya kupigwa faini.
Ni Tff hii hii iliyoshutumiwa kwamba mkataba wa mdhamini mwenza una walakini na Kuna uovu nyuma ya pazia. Watetezi wa Tff hapa walikuwa wakina nani? ( Akili kichwani mwako).
Ni Tff hii hii mpaka leo haijatoa tamko lolote kuhusu mshabiki wa Coastal kupigwa kule Tanga tena hadharani na watu wanaofahamika kwa sura na majina pamoja na timu wanayoishabikia. Mpaka Leo hakuna angalau tu tamko kwamba yule shabiki alipatikana au alikufa?
Ni Tff hii hii ambayo mpaka Leo pamoja na kuvuliwa nguo hadharani na kuachwa uchi na mtu waliyemfungia kwa kutamka hadharani Mimi sio mwajiriwa wa Tff ni mwajiriwa wa Yanga na nitaitumikia Yanga bila kujali chochote na kweli akahudumu kama alivyotamka hakuna tamko lolote mpaka Leo. Sio Kwa aliyefanya au taasisi iliyomtuma kufanya. Au mnasubiri na Simba nao wateleze Ili mtoe adhabu kwa kubalance?
Ni Tff hii hii ambayo Kila mechi ya daby Yanga wanapita mlango pori na wamekaa kimya wakiipiga faini ya laki Tano mpaka million moja. Ni kama wamebariki tendo hilo Ili waje wapige faini. Nilidhani kama timu imekuwa ikipewa adhabu na inalipa huku ikilirudia kosa Hilo Hilo Kila iitwapo Leo. Basi lingetoka tamko Kali kukomesha jambo Hilo. Ila kwa kuwa wanaofanya ni Yanga na wapo juu ya sheria basi linakaliwa kimya.
Naupenda mtifuano huu Kwa kuwa unawaumbua Tff wenyewe kwa kulea uovu ambao tunakoelekea tutafikia MCHELEA MWANA KULIA HULIA YEYE.
Natamani Yanga wasilegeze kamba Ili wawaumbue kwa kuwalea wenyewe.
Natamani ifike siku Yanga waamue ukimwaga ugali namwaga mboga watutajie kwa hasira siri ya wao kuwa juu ya Tff. Kama Kuna nini huwa wanafanya mpaka wanaogopwa kiasi hicho ni muhimu waweke hadharani Ili tujue MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.
TFF KWENYE SAKATA HILI HAKUNA WA KUMLAUMU ILA NI TFF WENYEWE.
(Jicho la tatu la Mgalilaya).