Phone4Sale Nauza iPhone 11

kwahiyo na iphone 14 pro max kioo chake ni cha bei rahisi ndio maama inakaa na chaji sana ?
naomba ujibu hayo masuali yangu
Nilikuwa ninaongelea iPhone 11 sio 14 Pro Max. Hiyo iPhone 14 Pro Max unayoiulizia ina betri kubwa la 4323mAh na bado chipset inayotumia (Bionic A16) ina ulaji mzuri wa chaji hivyo inafanya iPhone 14 Pro Max itunze sana chaji licha ya kuwa na kioo cha ubora wa hali ya juu. Nilichokuwa najaribu kuelezea ni kwamba kioo cha iPhone 11 ni cha kawaida sana ukilinganisha na bei yake. Vioo vya bei rahisi haviconsume power kubwa kama vile vioo expensive

Pia kama ulivyoambiwa, wewe focus na kuuza simu, sikutaka tufike huku
 

usiwe na haraka twende taratibu
kwahiyo iphone 11 (Bionic yake unajua ) vp ni sawa na iyo x max ? naomba jibu hapa usipanic
pili juu nimekuliza maswali mawili umejibu 1
naomba ujibu hili ujibu la lile la juu
 
usiwe na haraka twende taratibu
kwahiyo iphone 11 (Bionic yake unajua ) vp ni sawa na iyo x max ? naomba jibu hapa usipanic
pili juu nimekuliza maswali mawili umejibu 1
naomba ujibu hili ujibu la lile la juu
Swali lako sikuliona. Umeuliza je, display na camera ndio vitu pekee vya kuonesha ubora WA simu? Jibu ni hapana lakini ni vipengele muhimu sana kuliko vingine

Kwa mfano ona hapa[emoji116][emoji116]
*iPhone 11 inatumia chipset ya Bionic A13 na iPhone XS Max inatumia Bionic A12. Licha ya A13 kuwa na performance kubwa kuliko A12 lakini zote zimetengenezwa kwa process ya 7nm na in real life performance zake zinafanana na utofauti wake ni mdogo Sana. Hakuna massive improvement hapa
*iPhone 11 inatunza chaji kuliko iPhone XS Max, Kuna vitu kadhaa vimepelekea iwe hivi lakini sababu kubwa ni display. Kwenye iPhone 11 Apple ametumia panel za ubora wa chini sana ukilinganisha na bei yake. Kioo cha iPhone 11 hakili Sana chaji kama cha iPhone XS Max kwa sababu ni cha ubora wa chini

Lakini ukija sehemu ambazo iPhone XS Max ipo juu ya iPhone 11 utofauti ni mkubwa Sana.
iPhone XS Max ina 2× optical zoom na iPhone 11 haina kabisa. Pia iPhone XS Max ina telephoto camera Ila iPhone 11 haina hii kitu
Kwenye display sasa ndio utofauti mkubwa unapojionesha. Kioo cha iPhone 11 kinapitwa hadi na simu za laki 5 kwa ubora. Display ni part ya simu ambayo ni lazima uitumie na muda wote ukiwasha simu unatumia display. Hata ukiziweka iPhone 11 na iPhone XS Max meza moja na ukaziwasha utaona kuwa iPhone XS Max ina kioo premium Sana, na iPhone 11 kioo chake hakina maajabu yoyote licha ya kuuzwa kwa bei kubwa (laki moja na nusu zaidi ya iPhone XS Max)

iPhone 11 ina improvements chache sana kwenye performance ukilinganisha na iPhone XS Max lakini ina downgrade kubwa Sana kwenye display ukilinganisha na iPhone XS Max
 

Asante nimefurahi kulitambua hilo kujibu (HAPANA)
ukweli ni kwamba iphone 11 ni advance ya XS Max
na pia umekubali perfomance yake ni kubwa kuliko XS
kipengele kikubwa ni perfomance na ndio maana inapokea matoleo mengi kuliko XS max
kwahiyo itoshe kusema iphone 11 ni kubwa kuliko hiyo



Asante kwa maelezo mengi majibu machache
 
iPhone XS Max ni nzuri kuliko iPhone 11
Period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…