Nauza kuku wa mayai ambao sasa wamegeuka wa kienyeji, jipatie mbegu na nyama bora hapa

Nauza kuku wa mayai ambao sasa wamegeuka wa kienyeji, jipatie mbegu na nyama bora hapa

Mjasiriamali M

Senior Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
142
Reaction score
69
Habari za leo wadau,

Nimekuwa na Kuku wa Mayai Kwa Mwaka Sasa, wametaga kiasi chake ingawa kwa kipindi cha mwezi sasa wamesitisha kutaga, so tangu walipoamua kugoma huko nami nimewabadilishia mazingira ya kutoka Uzungu na kuwa Uswahili, NOW wanakula Mostly Pumba na mabaki ya vyakula vya nyumbani, kikubwa zaidi nina mtu ananiletea Viroba viwili vikubwa vya mabaki ya mbogamboga zote toka sokoni ambazo wao huita uchafu while kwa hawa kuku ni msosi tosha, Hii Imewasaidia kuwapa afya nzuri na kinga maana nna zaidi ya mwezi na nusu sijaona kuku aliepooza au kujitenga na wenzie (Kwa Ugonjwa).

Mayai yao kwa sasa yanatoa kiini cha njano kiasi kwamba ukiyapiga na chipsi yai mtu hudhani ni ya kienyeji pure.

Kwa sasa nna waauza hawa kuku kwa bei poa kabisa ili nisafishe banda na kuingiza kuku wengine, kwa wale wanaohitaji kupata mbegu ya kuku mchanganyiko, njoo jipatie hawa majike ni wazuri na nna imani watakuzalishia tu, Pia kwa upande wa nyama kuku hawa wana ladha nzuri kama ya kuku wa kienyeji na mifupa yao ni migumu na Imara.

Bei ya Jumla ni Tsh Elfu 8 Tu na Reja Reja ni Tsh Elfu 10 Tu. Jumla ni Kuanzia Kuku 5.

Pia kwa wale wa Maofisini Unaweza ukasema unahitaji wangapi, TUNAKUCHINJIA NA KUMSAFISHA VIZURI, anawekwa ktk Fridge anaganda na unaletewa Nyama Ofisini au Popote Utakapo Hitaji, Hii Utalipia Nauli ya ziada (ambapo kuku mmoja hufikia Elfu 13)

Tuwasiliane Ili Tuongee Biashara Vizuri, Kuku wapo Tandika Maghorofani Karibu na Chuo cha Bandari na Utalii.

Shukrani.

0719 44 72 04.

. IMG_20150815_110445.jpgIMG_20150815_110511.jpgIMG_20150815_110725.jpgIMG_20150815_110656.jpg
 
Hahahaha.................Kiongozi hawa kuku wako ni kiboko, wamegeuka kutoka kisasa kwenda kienyeji baada ya kubadilisha ulishaji? Mh! Hii inabidi iingizwe kwenye maajabu ya dunia.
 
Back
Top Bottom