Nauza Layers Wanaotga

Nauza Layers Wanaotga

ndaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2013
Posts
347
Reaction score
49
Wadau nauza layers wangu wanataga kwa miezi 4 sasa..wapo 850 nauza 8000 kwa kila 1...niko morogoro lakini naweza kuwaleta popote.Nabadili biashara kwa kufuga zaidi machotara kwa ajili ya kutotolesha vifaranga na wa kienyeji.No yangu ni 0659300000 au ni PM.Thanks
 
Dar kisutu Layers wanauzwa kwa 7,000 as of now.

Risk kwa mnunuzi:-

1. Ni vigumu mfugaji kununua kwako sababu hajui hao kuku uliwatunzaje toka mwanzo hadi sasa
2. Ni vigumu kujua hao kuku ni wako kweli au umewapata kutoka vyanzo vizivyokuwa rasmi ikaleta shida baadaye!!

Utawauza lakini si kwa wafugaji makini - pole kukuambia hivyo.
 
Asante Fuso lakini maswali yako yanajibika vizuri
1.Mimi ninaranch ya kufugia ambayo iko registered kabisa hapa Morogoro kwani nafuga mifugo mingi ya aina mbali mbali
2.Records na reveipts za nilikonunua yaani Mkuza ninazo kwahiyo hakuna neno
3.Sintopenda kuwauza kwa wachinjaji kwabi hawa kuku bado wanataga yaani wako katika mwezi wao wa 4 katika kutaga
Kwa walio Morogoro karibuni kuja kuwaona
 
mkuu hebu toa ufafanuzi kuhusu swali la kwanza la mdau FUSO hapo juu, lina maana sana kwa anayetaka kuwafuga
 
Last edited by a moderator:
nipo Mpwapwa (chuoni, nasoma mifugo). je unaweza ukaniwekea kama 40 hivi hadi June 22 ndio nije niwachukue kwa sababu muda huo ndo nitakua likizo na nitaweza kuwafuga?
 
je ikiwa biashara yako inakupa faida kwa nn ubadilishe?
Toa maelezo ya ni kwajinsigani layers hawakulipi?, maana ni jambo jema ukiona biashara haikulipi unahamia nyingine, ila ni vema zaidi kueleza sababu za kutokukulipa kuliko kuwapa wenzio matatzo.
Isijeikawa ni 'culling method'
 
Je kuku wako 850 wanataga kwa asilimia ngapi?? Yaani Tray ngapi kwa siku??
 
Jamani msome maelezo yake kajieleza vizuri tu, kuku wanataga umri anazo risiti za Mkuza farm, kasema sababu anabadili biashara. Hayo ya faida nafikiri mnunuzi ni juu yako kufanya utafiti. Mimi ningekuwa tayari ningenunua ku test soko lake kuliko kuanza na vifaranga. All the best Ndaha
 
Back
Top Bottom