Kwa wasiokuwa na uelewa mzuri wa aina za mchele, kuna aina kuu mbili za mchele yaani mchele unaotokana na mpunga unaochukua miezi 3, na ambao unachukua miezi 6 toka kupanda hadi kukomaa.
Mchele unaokuwa kwa miezi 3 , yaani mpunga wa muda mfupi, huwa na mavuno mengi lakini ubaya wake hukatika sana wakati wa kukobolewa, hauna harufu nzuri, na ladha yake ni mbaya na huuzwa kwa bei chee sana mashambani.
Aina ya pili ni mchele unaotokana na mpunga unaochukua miezi 5 hadi 6 kukomaa, mchele huu una ladha nzuri na mtamu, unanukia kweeli kweli na pia huchambuka mmoja mmoja unapopikwa.
Kwa wafanyabiashara wengi wanaokusanya mpunga mashambani, kutokana na mpunga wa mbegu za muda mrefu kuwa ghali, basi huwa wanachanganya mchele huo na kuuingiza sokoni
Matokeo yake kwa mlaji huwa ni kila kitu kwa mbali na huwa unasumbua kupika hasa pale unapokuwa boko boko.
Kwa kulitambua hilo, mimi nina mchele wa miezi sita ambao haujachanganywa na kitu chochote maana nimeulima mwenyewe mkoani Morogoro.
Kwa wale wanaouza kidogo kidogo napokea order kuanzia kilo 100 kwa mikoa ya Dar, Tanga, Pwani, Lindi na Zanzibar.
Hakika utauuza kwa bei nzuri na kwa haraka sana.
Utaletewa sample kwa ajili ya makubaliano.
Ili kuepusha usumbufu wa simu, anaefanya biashara hii anicheki PM kwa maelewano ya bei.
NB: Mchele unafikishiwa ndio unatoa hela hatuna huduma ya kutuma.